BUSTANI YA WATU WEMA
وعن عائشة رضي اللَّه عنها قالت : سمِع رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم صَوْتَ خُصُومٍ بالْبَابِ عَالِيةٍ أَصْواتُهُمَا ، وَإِذَا أَحَدُهُمَا يَسْتَوْضِعُ الآخَرَ وَيَسْتَرْفِقُهُ فِي شيءٍ ، وَهُوَ يَقُولُ : واللَّهِ لا أَفعَلُ ، فَخَرَجَ عَلَيْهِمَا رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فقال : « أَيْنَ الْمُتَأَلِّي عَلَى اللَّه لا يَفْعَلُ المَعْرُوفَ ؟ » فقال : أَنَا يَا رسولَ اللَّهِ ، فَلهُ أَيُّ ذلِكَ أَحَبَّ . متفقٌ عليه
Kutoka kwa Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: Mtume ﷺ Alisikia sauti ya watu wakiteta Mlangoni wakiwa wamenyanyua sauti zao, Mmojawao alikuwa akimwomba mwenzie ampukunguzie (deni) na adai kwa upole, naye mwengine akisema “Wallahi sifanyi” : Mtume ﷺ Akawatokea na akawauliza
[Ni yupi aliyeapa kwa jina la Mwenyzi Mungu kuwa hatafanya wema?] Akasema: ni mimi Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nimempa khiyari afanye analopenda [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله