BUSTANI YA WATU WEMA
وعن أَبي زيدٍ أُسامة بْنِ حَارثَةَ ، رضي اللَّه عنهما ، قال : سَمِعْتُ رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يَقُولُ : « يُؤْتَـى بالرَّجُلِ يَوْمَ الْقِيامةِ فَيُلْقَى في النَّار ، فَتَنْدلِقُ أَقْتَابُ بَطْنِهِ ، فيَدُورُ بِهَا كَمَا يَدُورُ الحِمَارُ في الرَّحا ، فَيجْتَمِعُ إِلَيْهِ أَهْلُ النَّار فَيَقُولُونَ : يَا فُلانُ مَالَكَ ؟ أَلَمْ تَكُن تَأْمُرُ بالمَعْرُوفِ وَتَنْهَى عَنِ المُنْكَرِ ؟ فَيَقُولُ : بَلَى ، كُنْتُ آمُرُ بالمَعْرُوفِ وَلاَ آتِيه ، وَأَنْهَى عَنِ المُنْكَرِ وَآَتِيهِ » متفق عليه
Kutoka kwa Abuu Zayd Usaamah bin Zayd bin Haarithah Radhi za Allah ziwe juu yake Amesema: Nimemsikia Mtume ﷺ akisema: [Ataletwa mtu siku ya Qiyama na atiwe motoni. Matumbo yake yatatoka nje awe akizunguka nayo kama vile anavyozunguka punda katika kinu (anapokuwa anasaga) ” Watu wa motoni watakumkusanyikia na waseme: “Ee Fulani, mbona uko hivyo ? Si uliokuwa ukituamrisha mema na kutukataza maovu?” Naye atasema: “Ndio, nilikuwa nikiamrisha mema wala sifanyi na nilikuwa nikikataza maovu na nikiyaendea] [Imepokewa na Bukhari, Muslim]
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله