BUSTANI YA WATU WEMA
عن أُمِّ الْمُؤْمِنين أُمِّ الْحكَم زَيْنبَ بِنْتِ جحْشٍ رضي اللَّه عنها أَنَّ النَّبِيَّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم دَخَلَ عَلَيْهَا فَزعاً يقُولُ : « لا إِلهَ إِلاَّ اللَّه ، ويْلٌ لِلْعربِ مِنْ شَرٍّ قَدِ اقْتربَ ، فُتحَ الْيَوْمَ مِن ردْمِ يَأْجُوجَ وَمأْجوجَ مِثْلُ هذِهِ » وَحَلَّقَ بأُصْبُعه الإِبْهَامِ والَّتِي تَلِيهَا . فَقُلْتُ: يَا رسول اللَّه أَنَهْلِكُ وفِينَا الصَّالحُونَ ؟ قال : « نَعَمْ إِذَا كَثُرَ الْخَبَثُ » متفقٌ عليه
Kutoka kwa Mama wa Waumini Ummul Hakam Zaynab bint Jahsh Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba: Mtume ﷺ aliingia kwake akiwa amefadhaika, huku akisema: [Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu mmoja tu. Ole wao Waarabu! kwa shari iliyokaribia. Imefunguliwa leo tundu (katika ukuta unaowazuia) Juju na Maajuj mfano wa huu] na akashiria mzunguko kwa vidole vyake kwa kutumia kidole gumba na kile kinachofuata. ” Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tutaangamizwa na miongoni mwetu kuna watu wema? Akasema: [Ndio, pindi maovu yatakapokithiri.] [Imepokewa na Bukhari]
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله