BUSTANI YA WATU WEMA
{وقال تعالى : {فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ
{وقال تعالى : {مَّا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِن شَيْءٍ
{وقال تعالى : {فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ
{وقال تعالى : {وَأَنَّ هَٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ
{وقال تعالى : {قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ
والآيات في الباب كثيرة معلومة
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[Na kipo kitu gani baada ya haki, isipokuwa upotovu tu?] [Suurat Yunus:32]
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote] [Suurat An’aam:38]
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume] [Surat An-Nisaai:59]
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake.] [Suurat An’aam:153]
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu] [Suurat Al ‘Imran:31]
Na Aya katika Mlango huu ni nyingi zenye kujulikana.
شرح مقدمة الباب مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله