BUSTANI YA WATU WEMA
وعن ابنِ عباسٍ رضي اللَّه عنهما أَنَّ رسُولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم لَقِيَ ركْباً بالرَّوْحَاءِ فقال: «مَنِ الْقوْمُ ؟ » قالُوا : المُسْلِمُونَ ، فَقَالُوا : مَنْ أَنْتَ ؟ قال : «رسولُ اللَّه» فَرَفَعَتْ إِلَيْهِ امْرَأَةٌ صَبِيًّا فَقَالَتْ : أَلَهَذَا حَجٌّ ؟ قال : « نَعمْ وَلَكِ أَجْرٌ » رواه مسلم
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alikutana na Msafara fulani kutoka (sehemu inaoitwa) Rawhaa (karibu na Madina) akawauliza: [Ni watu gani Hawa ?] Wakasema: “Ni Waislamu.” na wao wakamuliza: “Wewe ni nani?” Akasema: [Mtume wa Mwenyezi Mungu.] Mwanamke mmoja (aliyekwepo) alimnyanyua mtoto mdogo na kuuliza: “Je,huyu ana hijja?” Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akamjibu : [Ndio, na wewe una ujira (kwa hilo).] [Imepokewa na Muslim ]
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله