0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

170. Riyadhu Swalihina Mlango wa kukataza Bid’a na mambo ya Uzushi Hadithi ya 02


BUSTANI YA WATU WEMA


1463655589


وعن جابرٍ، رضي اللَّه عنه ، قال : كان رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، إِذَا خَطَب احْمرَّتْ عيْنَاهُ ، وعَلا صوْتُهُ ، وَاشْتَدَّ غَضَبهُ ، حتَّى كَأَنَّهُ مُنْذِرُ جَيْشٍ يَقُولُ : «صَبَّحَكُمْ ومَسَّاكُمْ » وَيقُولُ : « بُعِثْتُ أَنَا والسَّاعةُ كَهَاتيْن » وَيَقْرنُ بين أُصْبُعَيْهِ ، السبَابَةِ ، وَالْوُسْطَى ، وَيَقُولُ: « أَمَّا بَعْدُ ، فَإِنَّ خَيرَ الْحَديثَ كِتَابُ اللَّه ، وخَيْرَ الْهَدْى هدْيُ مُحمِّد صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، وَشَرَّ الأُمُورِ مُحْدثَاتُهَا وكُلَّ بِدْعَةٍ ضَلالَةٌ » ثُمَّ يقُولُ : « أَنَا أَوْلَى بُكُلِّ مُؤْمِن مِنْ نَفْسِهِ . مَنْ تَرَك مَالا فَلأهْلِهِ ، وَمَنْ تَرَكَ دَيْناً أَوْ ضَيَاعاً، فَإِليَّ وعَلَيَّ »   رواه مسلم


Kutoka kwa  Jaabir Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Mtume  Alipokuwa akikhutubia macho yake yalikuwa yakibadilika rangi na kuwa mekundu, na akinyanyua sauti yake, na ghadhabu yake ikishitadi kana kwamba alikuwa anatahadharisha na jeshi la adui. akisema: [Adui atawashambulieni asubuhi na Jioni.] Na akisema: [Nimetumilizwa  mimi na Qiyam kama hivi.] akivishikanisha vidole vyake cha shahada na kidole cha kati, na akisema [Ama baada ya haya: “Hakika mazungumzo bora ni kitabu cha Mwenyezi Mungu na uongofu bora ni uongofu wa Mtume , na mambo yaliyomaovu ni yale yenyekuzuliwa na kila lenye kuzuliwa ni upotevu.]

Kisha alikuwa akisema: [Mimi ni mwenyekumtakia kila Muumin masilahi yake kuliko anavyojitakia nafsi yake, hivyo yoyote atayeacha mali ni kwa ajili ya watu wake, na yoyote atakayeacha deni au watoto na familia basi hayo yatakuwa juu yangu.]     [Imepokewa na Muslim]


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله



Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.