BUSTANI YA WATU WEMA
عنْ أَبِي عبدِ اللَّه النُّعْمَانِ بْنِ بَشيِرٍ رضي اللَّه عنهما، قال: سمِعْتُ رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقولُ : « لَتُسَوُّنَّ صُفُوفَكُمْ أَوْ لَيُخَالِفَنَّ اللَّه بَيْنَ وُجُوهِكمْ » متفقٌ عليه
وفي روايةٍ لِمْسلمٍ : كان رسولُ اللُّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يُسَوِّي صُفُوفَنَآ حَتَّى كأَنَّمَا يُسَوي بِهَا الْقِداحَ حَتَّى إِذَا رأَى أَنَّا قَدْ عَقَلْنَا عَنْهُ ثُمَّ خَرَجَ يَوماً ، فقامَ حتَّى كَادَ أَنْ يكبِّرَ ، فَرأَى رجُلا بادِياً صدْرُهُ فقالَ : « عِبادَ اللَّه لَتُسوُّنَّ صُفوفَكُمْ أَوْ لَيُخَالِفَنَّ اللَّه بيْن وُجُوهِكُمْ »
Kutoka kwa Abuu ‘Abdillaah, An-Nu’maan bin Bashiyr Radhi za Allah ziwe juu yake Nilimsikia Mtume ﷺ akisema: [Wa-Allaahi mtazisawazisha safu zenu au Mwenyezi Mungu Atazibadilisha nyuso zenu] [Imepokea na Bukhari na Muslim]
Na katika Riwaya nyingine ya Muslim imesema:
alikuwa Mtume ﷺ akizisawazisha safu kana kwamba alikuwa anasawazisha kwazo mshale, mpaka alipo tuona tumelifahamu hilo. Kisha siku moja akatoka, akasimama hata alipokaribia kupiga Takbiri, akamuona mtu kifua chake kimetokeza, akasema: [Enyi waja wa Mwenyezi Mungu, mtasawazisha safu zenu au Mwenyezi Mungu Atazibadilisha nyuso zenu]