BUSTANI YA WATU WEMA
وعن أَبِي ربْعِيٍّ حنْظَلةَ بنِ الرَّبيع الأُسيدِيِّ الْكَاتِب أَحدِ كُتَّابِ رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : لَقينَي أَبُو بَكْر رضي اللَّه عنه فقال : كَيْفَ أَنْتَ يا حنْظلَةُ ؟ قُلْتُ : نَافَقَ حنْظَلَةُ ، قَالَ : سُبْحانَ اللَّه ما تقُولُ ؟، : قُلْتُ : نَكُونُ عِنْد رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يُذكِّرُنَا بالْجنَّةِ والنَّارِ كأَنَّا رأْيَ عين ، فَإِذَا خَرجنَا مِنْ عِنْدِ رسولِ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم عافَسنَا الأَزْوَاجَ وَالأَوْلادَ وَالضَّيْعاتِ نَسينَا كَثِيراً قال أَبُو بكْر رضي اللَّه عنه : فَواللَّهِ إِنَّا لنَلْقَى مِثْلَ هَذَا فانْطلقْتُ أَنَا وَأَبُو بَكْر حتى دخَلْنَا عَلى رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم . فقُلْتُ نافَقَ حنْظَلةُ يا رسول اللَّه ، فقالَ رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: « ومَا ذَاكَ؟» قُلْتُ: يا رسولَ اللَّه نُكونُ عِنْدكَ تُذَكِّرُنَا بالنَّارِ والْجنَةِ كَأَنَّا رأْيَ العَيْنِ فَإِذَا خَرَجْنَا مِنْ عِنْدِكَ عَافَسنَا الأَزوَاج والأوْلاَدَ والضَّيْعاتِ نَسِينَا كَثِيراً . فقال رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: «وَالَّذِي نَفْسِي بِيدِهِ أن لَوْ تَدُومُونَ عَلَى مَا تَكُونُونَ عِنْدِي وَفِي الذِّكْر لصَافَحتْكُمُ الملائِكَةُ عَلَى فُرُشِكُم وفي طُرُقِكُم ، وَلَكِنْ يا حنْظَلَةُ ساعةً وساعةً » ثَلاثَ مرَّاتٍ ، رواه مسلم
Kutoka kwa Abuu Rabi’y, Handhwalah bin Ar-Rabiy’ Al-Usayyidiy ambaye ni mmoja katika waandishi wa Mtume ﷺ amesimulia: “Siku moja Abuu Bakar Radhi za Allah ziwe juu yake alikutana nami, akaniuliza: Vipi hali Ewe Handhwalah? Nikamwambia: “Handhwalah anajikhofia unafiki! Akasema: Subhaana Allaah! Umesema nini? Nikamwambia: Sisi huwa tupo mbele ya Mtume ﷺ akitukumbusha Pepo na moto kana kwamba huwa tukiziona. Lakini tunapoondoka kwa Mtume ﷺ hushughulika na wake zetu na watoto wetu na shughuli za kuendesha maisha yetu, hivyo hutufanya tusahau mengi. Abuu Bakar Radhi za Allah ziwe juu yake akasema: Wa-Allaahi nasi pia hukutana na hali kama hii. tukaondoka Mimi na Abuu Bakar tukaingia kwa Mtume ﷺ nikamwambia: Handhwalah anajikhofia unafiki Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tunapokuwa kwako unatukumbusha moto na Pepo kana kwamba tunaziona kwa macho, tunapoondoka kwako, hushughulika na wake zetu na watoto wetu na shughuli za kuendesha maisha yetu, hivyo hutufanya tusahau mengi. Mtume ﷺ akasema: [Naapa kwa Ambaye nasfi yangu ipo mikononi Mwake, lau mnadumu katika hali mnayokuwa nayo kwangu na katika kumtaja Mwenyezi Mungu, basi Malaika wangewasalimia nyinyi mnapokuwa vitandani mwenu na njiani. Lakini Ewe Handhwalah, ni saa na saa (kuna wakati wa kutekeleza ‘ibada na kuna wakati wa kuangalia mambo ya maisha.)] Alikariri hivyo mara tatu. [Imepokewa na Muslim]
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله