BUSTANI YA WATU WEMA
قال اللَّه تعالى : {وَالَّذِينَ جَاهَدُوا فِينَا لَنَهْدِيَنَّهُمْ سُبُلَنَا ۚ وَإِنَّ اللَّهَ لَمَعَ الْمُحْسِنِينَ} العنكبوت:69
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[Na wanao fanya juhudi kwa ajili yetu, Sisi tutawaongoa kwenye njia zetu. Na hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na watu wema] [Suurat Al A’nkabut:29]
99:وقال تعالى :{وَاعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأْتِيَكَ الْيَقِينُ} الحجر
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini.] [Suuratul Hijr:99]
8:وقال تعالى :{وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ وَتَبَتَّلْ إِلَيْهِ تَبْتِيلًا} المزمل
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[Na lidhukuru jina la Mola wako Mlezi, na ujitolee kwake kwa ukamilifu.] [Surat Al-Muzzammil:8]
20:وقال تعالى :{وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللَّهِ هُوَ خَيْرًا وَأَعْظَمَ أَجْرًا ۚ } المزمل
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[Na kheri yoyote mnayo itanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Mwenyezi Mungu, imekuwa bora zaidi, na ina thawabu kubwa sana.] [Surat Al-Muzzammil:20]
215:وقال تعالى :{وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّهَ بِهِ عَلِيمٌ} البقرة
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[Na kheri yoyote mnayo ifanya Mwenyezi Mungu anaijua.] [Sura Al-Baqara:215]
والآيات في الباب كثيرة معلومة
Na aya katika Mlango huu ni nyingi zajulikana.
شرح مقدمة الباب مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى