June 25, 2021
0 Comments
BUSTANI YA WATU WEMA
وَعنْ أنَسٍ رضي اللَّهُ عنه قال : كَان أخوانِ عَلَى عهْدِ النبيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، وكَانَ أَحدُهُما يأْتِي النبيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، والآخَرُ يحْتَرِفُ ، فَشَكَا الْمُحْتَرِفُ أخَاهُ للنبيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فقال : « لَعلَّكَ تُرْزَقُ بِهِ » رواه التِّرْمذيُّ بإسناد صحيح على شرط مسلمٍ
« يحْترِفُ » : يكْتَسِب ويَتَسبَّبُ
Kutoka kwa Anas Radhi za Allah ziwe juu yake amesema:Kulikuwepo ndugu wawili zama za Mtume ﷺ, mmoja alikuwa akienda kwa Mtume ﷺ (na kukaa naye), na mwengine anafanya kazi; yule anayefanya kazi akamshitakia Mtume ﷺ dhidi ya ndugu yake, Mtume ﷺ akamwambia: [Pengine wewe unaruzukiwa kwa sababu yake.] [Imepokewa na At-Tirmidhiy kwa isnaad Sahihi]