SOMO LA FIQHI
WAKATI WA KUTOLEWA ZAKA
Wakati bora wa kutoa zaka za fitri ni kutoa siku ya idd baada ya kutokeza kwa alfajiri na kabla ya swala ya Idd, na yaruhusiwa kutanguliza kuitoa kwa siku moja au siku mbili kabla siku ya Idd; kwa utkelazaji wa maswahaba. Wala haifai kuichelewesha hadi baada ya swala ya Idd, kwa Hadith ya Ibn Umar radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume
[أن النبي صلى الله عليه وسلم أمر بزكاة الفطر أن تؤدى قبل خروج الناس إلى الصلاة]
[Ameamrisha Zaka za Fitri na zitolewe kabla ya watu kutoka kuswali (Iddi)]
Na katika Hadith ya Ibn Abbas Radhi za Allah ziwe juu yake: Amesema Mtume
[من أداها قبل الصلاة فهي زكاة مقبولة، ومن أداها بعد الصلاة فهي صدقة من الصدقات] رواه أبوداود
[Atakayeitoa kabla ya swala basi ni Zaka inayokubaliwa, na atakayeitoa baada ya swala basi ni sadaka miongoni mwa sadaka] [Imepokelewa na abi daud.]