0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

UTANGULIZI WA WALIO ONGOKA

UISLAMU NI DINI YA MANABII WOTE

Sifa zote njema ni zake Allah,Muumba wa mbingu na ardhi,Muumba wa vinavyoonekana na visivyoonekana, Allah ambaye amemtuma Mtume ﷺ kwa uongofu na kwa Dini ya Haki ili ajaaliye ishinde dini zote japo kuwa watachukia makafiri. Rehma na amani zimwendee Mume ﷺ, na Familia yake Tukufu,maswahaba wake watukufu, na wote waliomfuata hadi siku ya malipo Ameen.

Tunamshukuru Allah [swt] aliye tuumba sisi kuwa wanadamu,wala sio wanyama, na akatujaalia akili ili tuchanganue mema tuyafuate, na mabaya tuyaepuke, na juu ya yote Tunamshukuru Allah [swt] aliye tujaalia sisi kuwa Waislam wanaomwabudu pasina kumshirikisha na viumbe vyake au madai yasiyo ingia akilini.vile vile tunamshukuru Allah[swt] kuwa katika ummati Muhammad ﷺ.

Uislam ni Dini iliyokamilika kwa Nyanja zote , na ni mfumo kamili wa maisha. Uislam umejengwa kwa nguzo tano muhimu, shahada,sala,saumu,zakaa na hijja na vyote hivi vyalingania vitu viwili, Umoja na Tabia nzuri katika mazungumzo,ibaada, mavazi n.k, jambo ambalo ni muhali kwa madini yaliyosalia.

Ndugu msomaji,sisi waislam twawafundisha ndugu wakristu kwa Heshima ya Uislam,sio kwa dharau zao,tunakupa ukweli wa Quraan wala siyo propaganda ya vitabu vyao,tunakupeni maandiko kwa haki na usahihi, wala siyo chuki inayobainika kwa midomo yao. Mara nyingi wao huongeza au kupunguza maneno ya Allah [swt] ili kutafuta faida za kidunia [Quraan 2:79], sisi twakutakieni paradise na insha Allah ujumbe utakufikieni.

Kila tunapokuwa katika kutoa darsa,mahubiri au mafundisho, lazima kutoa ushahidi, ni lazima uwe mkweli kwa nafsi yako kwanza unapo soma Maandiko Matukufu, wazungu wanasema,  “If quoting Maintain Accuracy, If Claiming Provide Proof ”  na mara nyingi wengi katika ndugu wakristu hawazingatii misingii hii muhimu ya mazungumzo! Mazungumzo ni njia ya kupeana fikra , na lazima upendo udhihirike, lakini kwa kumtukana Allah [swt], Mtume ﷺ pamoja na Waislam, sidhani kama kuna chochote kinachoweza kutuvutia.

Napenda ndugu wakristu wajuewazi kuwa Uislam ni Imani kuwa Mola ni Mmoja tu,na ndiye aliyeweka njia na mikakati maalum ya Ibaada na Maombi ambayo haikubali kamwe mifano au masanamu kwa namna yoyote. Katika Uislam Allah [swt] pekee ana uhai wa milele, na chochote kinachofikwa na al-maut hakiwezi wala hakifai kuabudiwa kwa namna yoyote ile, kwa hivyo uhusiano baina ya kiumbe na Muumba ni wa moja kwa moja wala hatuhitaji washenga kama walivyo ndugu wakristo, na Manabii wote ni waonyaji, viongozi na Mitume na wao pia walifanya Ibaada kwa Allah[swt] tena kwa bidii kubwa, na ndio ile Dua maarufu ya Rabbana aatina fiidunia hasana, wafil akheerati hasana ……………. .

Uislamu unakubali kuwa Muislamu aweza kushawishiwa na nafsi yake na akafanya uovu dhidi ya Allah [swt],au kuwakosea wanadamu wenzake, na kwa hili kila mmoja atachukua mzigo wake mwenyewe, wala hatuwezi kusema eti hayo ndiyo maamrisho ya Uislamu, kwa hivyo propaganda za wamagharibi,dola zetu na wakristu hazina athari kwa Uislamu na ndio sababu wamagharibi wengi wanaingia kwa Uislamu MAKUNDI MAKUNDI. Ndugu msomaji lengo la Uislamu ni kutoa mfumo kamili wa maisha bila kuacha sehemu yoyote ya maisha ya kiumbe huyu mwanadamu, naleo ndiye hasimu mkuu wa Allah [swt]

NA katika sehemu hii tutamulika wale watu mash’huri ulimwenguni waliopata nuru ya Uislamu na wakasilimu na kuweza Kuathiri wafuasi wao na wao kuwa waislamu.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.