0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

UTANGULIZI WA TWAHIDI

Tauhidi ndiyo aliyokuwa hali ya asili ya wanadamu na wala hawakuwa washirikina kwa dalili na ushahidi wa tarikhi (historia) na ushahidi wa fitra(hali na umbile la asili la wanadamu).

Kwanza: Dalili ya tarikhi kwamba tauhidi ndo asili
Kuna uzushi uliozuka kwamba wanadamu walikuwa washirikina katika asili yao, kisha wakaamrishwa kufanya tauhidi kwa dalili ya kuwa wanadamu walijua muingu wengi sana kuanzia kitambo kisha wakajua kumpwekesha Mwenyezi Mungu baadaye. Lakini hii si kauli ya kweli kwa dalili zifwatazo:

1. Lengo kubwa la kuumbwa Adam (a.s) lilikuwa kwamba amuabudu Mwenyezi Mungu kama alivyosema Allah:

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ}     الذاريات:56}

[Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.]       [Al-Dhariyaat:56]

2. Adam (a.s) ambaye ndiye baba wa wanadamu wote na Hawaa ambaye ndiye mama yao wote, walikuwa wanatauhidi kabla hawajakula katika mti uliokatazwa. Kisha wakatubia kwa Allah (s.w)kwa kusema : قالا رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنْفُسَنَا وَإِنْ لَمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ}    الأعراف:23}

[Wakasema: Mola wetu Mlezi! tumejidhulumu nafsi zetu, na kama hutusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa katika wenye kukhasirika.]       [Al-A’araaf:23]

3. Mwenyzi Mungu (s.w) alimchagua Adam (a.s)baina ya viumbe wake wote, na Mwenyezi Mungu hamchagui mshirikina.Amesema Mwenyezi Mungu:

[ إِنَّ اللَّهَ اصْطَفَى آدَمَ وَنُوحًا وَآلَ إِبْرَاهِيمَ وَآلَ عِمْرَانَ عَلَى الْعَالَمِينَ]

[Hakika Mwenyezi Mungu alimteuwa Adam na Nuhu na ukoo wa Ibrahim na ukoo wa Imran juu ya walimwengu wote.]      [Al-Imran 33]

Pili: Dalili ya fitra (umbile la asili la viumbe) kwamba tauhidi ndo asili
Nalo ni lile umbile alilowaumba Mwenyezi Mungu viumbe kwalo, kwani aliwaumba huku wakikiri kwamba Yeye Mwenyezi Mungu yupo na kwamba Yeye ndiye aliyewaumba hapa mwengine. Haya ni kwa dalili zifuatazo:
1. Tokea Allah alipowaumba viumbe, aliwaumba huku wakikiri kuwa Yeye Allah ndiye Mola wao Mlezi Muumba wa kila kitu na anayestahiki kuabudiwa kwa haki. Amesema Allah s.w:

 وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِنْ بَنِي آدَمَ مِنْ ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَى أَنْفُسِهِمْ أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ قَالُوا بَلَى شَهِدْنَا أَنْ تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَذَا غَافِلِينَ، أَوْ تَقُولُوا إِنَّمَا أَشْرَكَ آبَاؤُنَا مِنْ قَبْلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةً مِنْ بَعْدِهِمْ أَفَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ الْمُبْطِلُونَ      الأعراف:172

[Na pale Mola wako Mlezi alipo waleta katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao, na akawashuhudisha juu ya nafsi zao, akawaambia: Je, Mimi si Mola Mlezi wenu? Wakasema: Kwani! Tumeshuhudia. Msije mkasema Siku ya Kiyama sisi tulikuwa tumeghafilika na hayo.]    [Aaraf 172]

2. Mwenyezu Mungu pia ameeleza kuwa amewaumba waja wake hunafaa(waongofu)huku wakimfanyia Yeye dini peke yake, kwani hiyo ndiyo inayoitifaki (kuafikiana)hali ya asili aliyowaumba wao na akachukua ahadi yao katika mgongo wa baba yao Adam (a.s). Amesema Allah katika hadithi qudsi:

[ وإني خلقت عبادي حنفاء كلهم، وإنهم أتتهم الشياطين فاجتالتهم عن دينهم، وحرمت عليهم ما أحللت لهم، وأمرتهم أن يشركوا بي ما لم أنزل به سلطانا]

[Na hakika mimi nimeaumba waja wangu (hali ya kuwa ni)waongofu wote. Na hakika wao walijiwa na mashetani basi wakawatoa kwa dini yao na wakawaharamishia yale niliyowahalalishia na wakawaamrisha kuwa wanishirikishe Mimi kwa vile ambavyo sikuwateremshia hoja yoyote]

3. Amesema Mtume ﷺ kuwa kila mzaliwa huzaliwa katika fitra:

 ما من مولود إلا يولد على الفطرة. فأبواه يهودانه وينصرانه ويمجسانه. كما تنتج البيهمة بهيمة جمعاء. هل تحسون فيها من جدعاء؟ )). ثم يقول أبو هريرة رضي الله عنه راوي الحديث: واقرءوا إن شئتم: [ فِطْرَتَ اللَّهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا]   الروم: 30

[Hakuna mzaliwa ila huzaliwa kwa fitra (umbile asili la wanadamu), kisha wazazi wake wanamfanya kuwa Myahudi au Mnaswara au Majusi. Kama anavyozaa mnyama mnyama kamili (mzima asiye na upungufu). Je huwa mnahisi upungufu (wowote kwake huyu mnyama?), kisha Abu Huraira (radhi za Allah ziwe juu yake) akasema: “someni ikiwa mnataka”: [Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini – ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilo waumbia watu.]   [Ar-rum 30]

Tatu: Dalili ya kuwa shirki haikuwa asili
1. Amesema Ibn Abbas (radhi za Allah ziwe juu yake) katika aya hii:

  كَانَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَة} [البقرة: من الآية 213] : “كان بين آدم ونوح عشرة قرون، كلهم على الإسلام    “أخرجه الطبري في تفسيره 2/ 334 والحاكم في المستدرك 2/ 442

[Walikuwa watu umma mmoja]   [Suratul-Baqara aya 213]   [Ilikuwa baina ya Adam na Nuhu (mada wa) karne kumi, wote hao walikuwa katika Wisilamu]   Imepokelewa na Twabary katika tafsiri yake 2/334 na Haakim katika Al-Mustadrak 2/442


Begin typing your search above and press return to search.