0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

UMOJA WA KIISLAMU SEHEMU YA TATU

UMOJA WA KIISLAMU SEHEMU YA TATU

Tulizungumza katika sehemu ya pili mambo yenye kutilia nguvu umoja wa kiislamu ,tukasema kuwa ni umoja katika itikadi (imani ) na tukafafanua kwa kadri tulivo afikiwa na mwenyezimgu sub hana hu wa taala.

Leo tukizungumzia jambo lengine lenye kutilia nguvu Umoja katika Uislamu;

UMOJA WA SHERIA NA SHAAIR (ALAMA ,NEMBO, VITAMBULISHI)

Ukitazama mambo yote wanao yafanyia kazi waislamu katika mambo yao ya kiibada utaona kuwa hakuna tofauti katika misingi ya utekelezaji wa mambo yenyewe, vilevile katika mambo ya kuhukumiana kwao.Mwenyezi Mungu anasema:

{شَرَعَ لَكُم مِّنَ الدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰ ۖ أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ}

[Allah anasema :amekuamrisheni dini ile aliyo muusia nuhu na tulio kufunulia wewe ,na tulio wausia Ibrahim na musa na issa ,kwamba shikamaneni na dini wala msifarikane kwayo.]    [shuraa: 13]

Anasema Sheikh Al Saady Allah amrehemu:”Na miongoni mwa ijtimai katika dini ni kuto tafautiana ni yale mambo yalio amrishwa na sharia katika mikusanyiko ya pamoja kama mikusanyiko ya ibada ya hajj ,idi mbili ,swala tano ,na jihad na mengineo katika mambo ya ibada ambayo hayawezi kukamilika ispokuwa kwa kuwa pamoja”.
Allah ameweka sheria kwa waislamu katika dini mambo ambayo yatakuwa ni yenye kuwakurubisha waumini kwa mola wao na kumtukuza ,miongoni mwa sheria hizo tukufu ni nguzo tano za uisilamu, kama ilivo pokewa na ibnu umar anasema ,anasema Mtume ﷺ:

 [بُنَي الإسلامُ على خَمْسٍ : شهادَةِ أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمَّداً رسولُ اللهِ، وإقَامِ الصَّلاةِ، وإيتَاءِ الزَّكاةِ، وحَجِّ البَيْتِ، وصَوْمِ رَمَضَانَ]        رواه البخاري

[Uislamu umejengwa kwa mambo matano, shahada mbili , swala ,zaka, hajj na swaumu ya mwezi wa ramadhani.]       [Imepokewa na Bukahri]

Na nguzo hizi tano zina muhusu kila Muislamu na Allah ameweka sheria kwa nguzo hizi ili kuthubitisha nguvu za Umma wa Kiislamu na mshikamano na kusaidiana kati yao.kama ambavyo sheria hizi ni upeo wa uzuri na uwadilifu na umoja kwa lengo la kuwapangia maisha na kupata mafanikio ya maisha ya Duniani na Akhera kwa Wanaadamu.
Pindi unapo tazama malengo matukufu ya sharia utaona kwa ujumla wake yapo kwa lengo la kuyathibitisha maslahi ya Umma wa Kiislamu kwa upande wa nguvu ,Umoja na kusaidiana kati yao, kwa mfano miongoni mwa malengo ya kuwekwa Sharia ya vita ni kuwasaidia wanyonge na kuondosha dhulma kati ya wanaadamu ,Allah anasema katika Qur’ani Tukufu:

وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَٰذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا

[Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako]      [Al Nnisaa:75]

Pia ukiitazama Ibada ya zaka utaiona kuwa ni faradhi inao wahusu wana jamii inaotoka katika nyoyo za Matajiri kwa lengo la kuwatakasa na uchoyo na ubakhili na kuyasafisha Mali yao,na hii ni njia pekee ilio faulu katika kupambana na ufukara ulio kithiri katika miji.
Vilevile katika utekelezaji wa ibada ya Swala kwa pamoja pia ibada ya Hajj ambapo Mahujaji wote wanaitikia mwito wa kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa sauti moja wakiwa katika viwanja vya Minaa na Arafa bila ya kutafautisha kati ya kiongozi (mfalme ) na raia na kati ya mweupe na mweusi na kati ya muarabu na asiekuwa muarabu.
Na katika kuzifanyia kazi Sharia hizi za Uislamu hakuna tofauti kati ya Mke na Mume,au Mkumbwa na Mdogo au kati ya Muungwana na Mtumwa,wote wapo sawa mbele ya Sharia ya Mwenyezi Mungu.kama ilivo pokewa katika hadithi ya Aisha kuhusu mwanamke wa kabila la Quraishi alieiba ,likawa kubwa jambo lake kwa kuwa atapishiwa hukumu ya kukatwa mkono na yeye ni mwanamke mtukufu jamaa zake wakamtuma Usama ili awaombee kwa bwana Mtume ﷺ hukumu hii iondoshwe kwa huyu mwanamke …Mtume ﷺ akakasirika mno akasema :

إِنَّمَا أَهْلَكَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ أَنَّهُ إِذَا سَرَقَ فِيهِمُ الشَّرِيفُ تَرَكُوهُ , وَإِذَا سَرَقَ فِيهِمُ الضَّعِيفُ قَطَعُوهُ , وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَوْ كَانَتْ فَاطِمَةُ ابْنَةُ مُحَمَّدٍ سَرَقَتْ لَقَطَعْتُ يَدَهَا

[hakika waliangamia walio pita kabla yenu alipo kuwa akiiba Mtukufu kati yao wakimuacha na anapo iba Mnyonge (asiekuwa na hadhi katika jamii) wakimsimamisha hukmu ,Wallahi napa kwa jina la Mwenyezimgu lau kama Fatima binti yangu angekuwa ndie alie iba ningemkata mkono wake.]    [imepokewa na Muslim]

Hii ndio sharia ya Mwenyezi Mungu imekuja kwa ajili ya Maslahi ya watu wote..
Itaendelea katika sehemu ya nne inshallah…

Imeandikwa na Hussein Ali Omar Swidiq

+255 717755358…+254 733666396

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.