TAREHE FUPI YA MJI WA MAKKA MTUKUFU
Tarehe ya Makka inakwenda nyuma hadi karne ya kumi na tisa kabla ya kuzaliwa Mtume Issa Alayhi salaam katika kipindi cha bwana wetu Ibrahim na Ismail, amani ziwashukie, kwani walikuwa ni watu wa mwanzo wa kukaa hapo. Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Anasema, Akimtolea hikaya Ibrahim:
رَّبَّنَا إِنِّي أَسْكَنتُ مِن ذُرِّيَّتِي بِوَادٍ غَيْرِ ذِي زَرْعٍ عِندَ بَيْتِكَ الْمُحَرَّمِ رَبَّنَا لِيُقِيمُوا الصَّلَاةَ فَاجْعَلْ أَفْئِدَةً مِّنَ النَّاسِ تَهْوِي إِلَيْهِمْ وَارْزُقْهُم مِّنَ الثَّمَرَاتِ لَعَلَّهُمْ يَشْكُرُونَ
[Mola wetu! Hakika mimi nimewakilisha watu wa nyumbani kwangu kwenye ardhi isiyokuwa na mazao, kwenye Nyumba yako tukufu, ewe Molawetu!, ili watekeleze Swala. Basi zifanye nyoyo za watu ziwaelekee wao kwa mapenzi na uwaruzuku matunda ili washukuru] [14: 37].
Na kwa fadhila ya dua ya bwana wetu Ibrahim u yalitembuka maji ya Zamzamu kutoka chini ya nyayo za Ismail u alipomalizikiwa na maji na chakula mama yake, Hajara. Na kutoka wakati huo, makabila yalikusudia kuja hapo kwenye maji, na mahali hapo pakaanza uhai.
Na makabila yakaendelea kuja hapo na kuzaana, mpaka utawala wa mahali hapo ukaja kwa Makureshi. Na Makureshi wakaendelea kutawala mpaka kudhihiri Nabii Mohammed ﷺ ambaye alikuwa na athari kubwa zaidi katika kugeuza maisha ya Makka tukufu na ulimwenguni kote.
Nabii Mohammed ﷺ alitumilizwa Makka, na Alkaba ikawa ni kibla cha Waislamu, na Makka ikawa ndio kituo cha ulinganizi wa Kiislamu, lakini watu wake walikuwa wakali zaidi katika kuwaepusha watu na Uislamu na kuwaadhibu waliosilimu, mpaka wakalazimika Waislamu kuhamia Madina iliyonawirishwa, na dola ya Kiislamu ikasimama huko. Kisha Mtume ﷺ akarudi Makka kuikomboa, ikawa kuanzia wakati huo, ni mji mkubwa wa Kiislamu mpaka zama zetu hizi.
Na kwahakika mji wa Makka ulipata umuhimu mkubwa kutoka kwa makhalifa na viongozi wakiislamu. Na wakajitolea kujenga Makka na kuupanua mji, na wakafanya makka ni kituo cha kusambaza nuru ya Dina ya Kiisalamu katika ulimwengu wote
UTUKUFU WA MJI WA MAKKAH
1. Ni amani kwa anayeingia
Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Anasema:
وَمَن دَخَلَهُ كَانَ آمِنًا} آل عمران:97}
[Na Mwenye kuingia atakuwa kwenye amani] [3: 97], Yaani Haramu ya Makka.
2. Haingi Masihi Dajjaal mji wa Makka, wala magonjwa hatari yenye kuambukiza na kuua.
Abu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake amepokewa akisema kwamba Mtume ﷺ alisema:
” الْمَدِينَة وَمَكَّة مَحْفُوفَتَانِ بِالْمَلَائِكَةِ عَلَى كُلّ نَقْب مِنْهُمَا مَلَك لَا يَدْخُلهُمَا الدَّجَّال وَلَا الطَّاعُون] أَخْرَجَهُ عُمَر بْن شَبَّة فِي ” كِتَاب مَكَّة]
[Madina na Makka imezungukwa na Malika, katika kila pembe [ Naqab: njia.] yake kuna Malaika. Haingiliwi na Dajjaal wala magonjwa hatari ya kuambukiza na kuua] [Imepokewa na umar bin shubbah].
3. Kuswali kwenye Msikiti wa Haram thawabu zake ni Swala elfu mia moja.
Jabir Radhi za Allah zimfikie yeye alipokewa akisema kuwa Mtume ﷺ alisema:
وَصَلَاةٌ فِي الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ أَفْضَلُ مِنْ مِائَةِ أَلْفِ صَلَاةٍ فِيمَا سِوَاهُ
[Swala moja ndani ya Msikiti wa Haramu ni bora kuliko Swala elfu mia moja katika misikiti mingine]
[Imepokewa na Ahmad na Ibnu Maajah.].
4. Makka ni ardhi inayopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
والله إنك لخير أرض الله وأحب أرضٍ إليَّ ولولا أن أهلك أخرجوني منك ما خرجت منك
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ: [Naapa kwa Mwenyezi Mungu! Wewe ni ardhi ya Mwenyezi Mungu njema zaidi, na ni ardhi ya Mwenyezi Mungu ninayo ipenda zaidi na lau watu wako hawangenitoa singetoka.] [Imepokewa Ahmad na Tirmidhi na Al-Nnasai.].
HUKMU ZINAZOHUSU MJI WA MAKKAH MTUKUFU
1. Onyo kali kwa anayetia nia kufanya ovu huko Haram, awe amelifanya au hakulifanya
Mwenyezi Mungu U Amesema:
{ وَمَن يُرِدْ فِيهِ بِإِلْحَادٍ بِظُلْمٍ نُّذِقْهُ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ} الحج:25
[Na yoyote mwenye kutaka kupotoka na kuleta udhalimu huko, basi tutamuonjesha adhabu kali] [22: 25].
Imepokewa na Ibn Abbas t kuotoka kwa Mtume ﷺ Akisema:
[أبغض الناس إلى الله ثلاثة: ملحد في الحرم] رواه البخاري
[Watu wanaochukiwa sana na Mwenyezi Mungu ni watu watatu) na akataja miongoni mwao ni (Mwenye kupotoka -kupinga Sharia ya Mwenyezi Mungu- katika Haram] [Imepokewa na Bukhari.].
2. Uharamu wa kupigana na kumwaga damu humo
Amesema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
{إِذْ جَعَلْنَا الْبَيْتَ مَثَابَةً لِّلنَّاسِ وَأَمْنًا} البقرة:125
[Na tulipoijaalia Nyumba ni mahali pa watu kukusanyika na mahali pa amani” [2: 125].
Mwenye kuingia Makka ataaminika humo, kwa neno la Mtume ﷺ:
[لا يحل لأحدكم أن يحمل السلاح بمكة] رواه مسلم
[Si halali kwa mmoja wenu kubeba silaha Makka] [Imepokewa na Muslim.].
Na amesema Mtume ﷺ:
إنّ مكّة حرّمها الله ولم يحرّمها النّاس، فلا يحلّ لامرئ يؤمن بالله واليوم الآخر أن يسفك بها دمًا ولا يعضد بها شجرةً] رواه البخاري
[Hakika Mwenyezi Mungu Ameiharamisha Makka na si watu walioiharamisha. Kwa hivyo, si halali kwa anayemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kumwaga damu huko wala kukata mti] [Imepokewa na Bukhari.]
3. Kuharamishwa kuingia makafiri na mushrikina haram ya Makka
Amesema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ فَلَا يَقْرَبُوا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ بَعْدَ عَامِهِمْ هَٰذَا} التوبة:28
[Enyi mlioamini! Hakika washirikina ni najisi, basi wasikaribie Msikiti wa Haram (Makka) baada ya mwaka wao huu] [9: 28].
Na Mtume ﷺ aliamrisha nayeye yuko Mina kutangazwe:
[لا يحج بعد العام مشرك ، ولا يطوف بالبيت عريان] رواه البخاري
[Asihiji mshirikina baada ya mwaka huu, na asitufu Al-Ka’ba mtu akiwa uchi] [Imepokewa na Bukhari.].
4. Uharamishaji wa kuwinda, kukata miti na kuokota kwenye Haram ila kwa mwenye kukijulisha
Ibnu ‹Abbas t alipokewa kutoka kwa Mtume ﷺ akisema:
إنّ الله حرّم مكّة فلم تحلّ لأحد قبلي، ولا تحلّ لأحد بعدي، وإنّما أحلّت لي ساعةً من نهار، لا يُختَلَى خلاها، ولا يعضَد شجرها، ولا ينفَّر صيدها، ولا تلتَقَط لقطتُها إلا لمعرّف رواه البخاري
[Mwenyezi Mungu Ameiharamisha Makka, si halali kwa yoyote kabla yangu wala kwa yoyote baada yangu. Mimi nilihalalishiwa kipindi kichache cha mchana. Mimea yake mibichi haikatwi, na pia miti yake haikatwi, na kiwindwa chake hakifukuzwi, na kilichopotea chake hakiokotwi isipokuwa kwa mwenye kukitangaza] [Imepokewa na Bukhari.].