SWALA YA KUPATA MWEZI NA JUA
Usiku na mchana kupishana ni miujiza ya Allâh ili mwanaadamu anufaike nayo, na Akajaalia iwe chini ya utumishi wake. Hakuna anayeweza kukhalifu kanuni ya mwendo wa jua na mwezi isipokuwa Allâh(Subhaanahu wa Taala)Peke Yake. Sababu za kimaumbile, Waumini na makafiri wote wanaikubali. Sababu za Sharia, Waumini wanazikubali na makafiri wanazikanusha. Na dalili ni Kauli ya Allâh(Subhaanahu wa Taala):
{وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ ۚ لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ} { فصلت:37}
“Na katika Ishara zake ni usiku na mchana, na jua na mwezi. Basi msilisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliye viumba, ikiwa nyinyi mnamuabudu Yeye tu.” [Al-Fuswilat:37]
Na Kauli YakeMwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
{ وَسَخَّرَ لَكُمُ الْفُلْكَ لِتَجْرِيَ فِي الْبَحْرِ بِأَمْرِهِ ۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ الْأَنْهَارَ} {إبراهيم:32}
“Na akafanya yakutumikieni majahazi yanayo pita baharini kwa amri yake, na akaifanya mito ikutumikieni.“ [Al-Ibrahim:32]
Na Kauli Yake Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Taala):
{وَآتَاكُم مِّن كُلِّ مَا سَأَلْتُمُوهُ ۚ وَإِن تَعُدُّوا نِعْمَتَ اللَّهِ لَا تُحْصُوهَا ۗ إِنَّ الْإِنسَانَ لَظَلُومٌ كَفَّارٌ} {إبراهيم:34}
“Na akakupeni kila mlicho muomba. Na mkihisabu neema za Mwenyezi Mungu hamwezi kuzidhibiti. Hakika mwanaadamu ni dhaalimu mkubwa, mwenye kuzikufuru neema.” [Ibrahim:34]
Na Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)Amesema:
{وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرٍّ لَّهَا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ} { يس:38}
“Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua.” [ Yasin:38]
Na Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala Amesema:
{لَا الشَّمْسُ يَنبَغِي لَهَا أَن تُدْرِكَ الْقَمَرَ وَلَا اللَّيْلُ سَابِقُ النَّهَارِ ۚ وَكُلٌّ فِي فَلَكٍ يَسْبَحُونَ} يس:40
“Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao.” [Yasin:40]
Abu Musa amesimulia: “Jua lilipatwa katika zama za Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam), akasimama huku akiwa amefazaika isije ikawa Qiyama kimesimama, akaenda Msikitini akasimama akiswali Swala yenye kisimamo kirefu, rukuu na sijda ndefu mno ambapo sijamuonapo akifanya hivyo katika Swala yoyote ile. Kisha akasema: [Alama hizi zinazotumwa na Allâh, huwa haziwi ni kwa kufa yeyote wala kuwa hai, bali Allah Anazituma Akiwahofisha waja Wake. Mtakapoona alama yoyote katika hizo, kimbilieni kumtaja Allah(Subhaanahu wa Taala), kumuomba dua na kumuomba istighfari]. [Imepokewa na Muslim.]
Kupatwa jua ni onyo la Mola juu ya kuepuka Sharia Yake. Mifano ya kukhalifu mafundisho ya Uislamu.
Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Taala)Amesema:
{وَلَوْ يُؤَاخِذُ اللَّهُ النَّاسَ بِمَا كَسَبُوا مَا تَرَكَ عَلَىٰ ظَهْرِهَا مِن دَابَّةٍ وَلَٰكِن يُؤَخِّرُهُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۖ فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ فَإِنَّ اللَّهَ كَانَ بِعِبَادِهِ بَصِيرًا} فاطر:45
“Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli wachukulia watu kwa waliyo yachuma, basi asingeli muacha juu ya ardhi hata mnyama mmoja. Lakini Yeye anawachukulia mpaka ufike muda maalumu. Basi ukifika muda wao basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake baraabara. [Fatir:45]
Jabir bin ’Abdullah (R.A) Amehadithia: “Jua lilipatwa katika zama za Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam siku yenye joto kali, Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam akawaswalisha Maswahaba zake, akarefusha kisimamo mpaka wakawa wakianguka, kisha akarukuu kitambo kirefu, akaitadili kitambo kirefu, akarukuu (tena) kitambo kirefu, akaitadili kitambo kirefu kisha akasujudu sijida mbili, akasujudu sijida mbili, kisha akasimama, akafanya kama alivyofanya mara ya kwanza. Ilikuwa ni Swala yenye rukuu nne na sijda nne. Nimeonyeshwa kila mahala mtakapoingia. Nikaonyeshwa Pepo, hata lau kama ningalichukua kichala (cha matunda) ningaliweza kukichukua. Nikaonyeshwa moto, nikamuona mwanamke wa Kiisraeli akiadhibiwa kwa sababu ya kumfungia paka ambaye hakumlisha wala hakumuacha aende akale vijidudu vya ardhini. Nikamuona Abu Thumama akiziburuta chango zake(matumbo)motoni. Watu walikuwa wakisema kuwa jua na mwezi havipatwi la kwa sababu ya kufa mtu mkubwa. Lakini hizo ni alama mbili za Allah Anawaonyesha, vitakaposhikwa, swalini mpaka viachwe.” [Imepokelewa na Muslim.]
Enyi umati wa Muhammad! Hakuna mwenye ghera kuliko Allah (Subhaanahu wa Taala) kumuona mja wake akizini, au mjakazi wake akizini. Enyi umati wa Muhammad! Lau mngalijua ninachokijua, mngalicheka kidogo na mkalia sana. Naapa kwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala), tangu niliposimama kuswali, niliona mutakayokutana nayo katika mambo ya dunia na Akhera yenu, hakuna ambacho sikukiona. Nimeyaona yote katika makamu yangu haya hata Pepo na moto. Nimeuona moto ukijitafuna wenyewe, sijaona mandhari ya kufazaisha kama leo. Nimemuona ’Amru bin Lahyi al-Khuzaiy akiburuta chango zake.
Nikamuona mwanamke akiadhibiwa kwa sababu ya paka, alimfungia wala hakumpa chakula wala hakumuacha aende akale vijidudu vya ardhini. Nimewaona jinsi mtakavyopewa mtihani makaburini mwenu, kama ule mtihani wa Dajjali atakapomjia mmoja wenu. Mtu ataulizwa: “ Mtu huyu unamjua vipi?” Muumini au mwenye yakini atasema: “ Ni Muhammad Mtume wa Allah, Alitujia na ubainifu na uongofu, tukamjibu, tukamuamini na tukamfuata.” hapo ataambiwa: “Lala ukiwa mwema. Tulikuwa tukijua kuwa ulikuwa ni mwenye yakini. Ama mnafiki au mwenye shaka, atasema: Simjui, niliwasikia watu wakisema kitu na mimi nikakisema!.