NI NINI UISLAMU?
Uislamu ni dini ya mwisho ambayo amekuja nayo bwana Mtume Muhammad S.A.W na Uislamu umekuja kukamilisha sheria zote zilizopita. Na uislamu ni dini ya Mitume wote kwanzia Adam mpaka Mtume Muhammad ﷺ.
Uislamu ni kunyenyekea na kujisalimisha kwa mungu na kumuabudu Mungu mmoja mwenye Nguvu alie Mbinguni.
MWENYEZI MUNGU NI NANI ?
Mungu au ALLAH ndie Mungu mmoja alieumba kila kitu na ndie anaeendesha kila kitu katika ulimwengu ni mungu mmoja anaejitegemea mwenye nguvu hakuzaa wala hakuzaliwa wala hafanani na kitu chochote wala haonekani kwa utukufu wake.
Mwenyzi Mungu anasema katika Qur’ani Tukufu Sura 112 Aya 1-4
[Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee.Mwenyezi Mungu MkusudiwaHakuzaa wala hakuzaliwaWala hana anaye fanana naye hata mmoja.]
UISLAMU UNAFUNDISHA NINI?
Uislamu unafundisha kumuabudu mungu mmoja na kuacha kuabudu Masanamu na vitu vingine , Uislamu unafundisha Tabia njema, kuishi na Majirani vizuri, kuwatendea wema wawili, na kuwafanyia wema watu wote hata wasiokua Waislamu imekuja katika Qur’ani Mwenyezi anasema:
[Hawakatazi Mwenyezi Mungu kwa wale wasiowapiga vita katika dini yenu na hawajawatoa katika majumba yenu kuwafanyia wema na kuwafanyia uadilifu hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wenye kufanya uadilifu]. [60:8]
YESU NI NANI KWA WAISLAMU?
Yesu ama Nabii (Issa) ni binadamu kama binadamu wengine na ni Mtume katika Mitume wa Mwenyezi Mungu wala sio mungu wala mwana wa mungu na kuzaliwa kwake bila ya baba ilikua ni Miujiza katika miujiza ya mungu kwani yesu ni kama Nabii (Adam) ambae aliumbwa bila ya Baba wala Mama.
[Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam; alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa! Basi akawa] [3:59]
Na Nabii Issa au yesu kama Manabii wengine alipewa Miujiza ya kufufua maiti na kuwaponya wagonjwa sio kwa uwezo wake bali ni kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho atawakana wanaomuabudu na sisi Waislamu tunaamini yakwamba yesu hakuuwawa wala hakusulubiwa bali alipaishwa Mbinguni kwa mwenyezi Mungu,na atashuka mwisho wa Dunia na kufariki.
[Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu – nao hawakumuuwa wala hawakumsalibu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini Bali Mwenyezi Mungu alim- tukuza kwake, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.] [4:157-158]