0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

NI MASHARTI GANI YA MTU KULAZIMIKA KUFUNGA?

NI MASHATRI GANI YA MTU KULAZIMIKA KUFUNGA?

Suali: Ni yapi Mashrti ya mtu kuwajibika Kufunga Mwezi wa Ramadhani ?

Jawabu: Masharti ya mtu kuwajibika Kufunga ni kama ifuatavyo:
1. Uislamu: Haimlazimu kafiri kufunga,na hata kama atafunga saumu yako haikubaliwi,na vile ile aliye ritadi amali zake hazukubaliwi,kwa neno lake Mwenyezi Mungu aliyetukuka:

{لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِين}    الزمر:65

“Bila ya shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu a’mali zako zitaanguka, na lazima utakuwa miongoni mwa wenye kukhasiri.”      [Al-Zzumar:65]

kwa sababu Uislamu ni Shari ya kukubaliwa amali ya Mwanadamu.

2. Kubaleghe: Sio lazima kwa mtoto mdogo kufunga, lakini huamrishwa kufunga akiwa anaweza ili kumpa mazoezi ya saumu naye azoee.Kwa neno lake Mtume ﷺ:

[رفع القلم عن ثلاثة: الصبي حتى يحتلم والنائم حتى يستيقظ والمجنون حتى يفيق.].     أخرجه أحمد وأبو داود

[Kalamu imeinuliwa juu ya watu watatu,Mtoto mpaka abaleghe,na alielala mpaka aamke,na Mwenda wazimu mpaka apoe]    [Imepokelewa na Ahmad na Abuu Daud]

3. Kuwa na akili: Sio wajibu kwa mwendawazimu kufunga.Kwa hadithi iliyo tangulia

4. Uwezo wa kufunga: Sio wajibu kufunga kwa mtu ambaye hawezi kufunga (labda amekuwa mzee sana ama afya yake haimruhusu kuhimili saumu).Kwa neno lake Mwenyezi Mungu aliyetukuka:

{وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ}      البقرة:184

“Na wale wasio weza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini.”

[Al-Baqara:184]

5. Kwa Mwanamke asiwe kuwa kwenye ada yake ya Mwezi, au damu yanifasi.ama akiwa katika ada yake ya mwezi au akiwa katika nifasi ni haramu kufunga na watalizimika kula na kulipa wakati mwengine kwa neno lake Bibi Aisha radhi za Allah ziwe juu yake asema:

[كنا نحيض على عهد رسول الله صلى الله عليه وسلم فنؤمر بقضاء الصيام ولا نؤمر بقضاء الصلاة]   رواه أبوداود

[Tulikuwa tukiingia kwenye hedhi zama za Mtume ﷺ tukiamrishwa kulipa Saumu wala hatuamrishwi kulipa Swala]    [Imepokewa na Abuu Daud]

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.