0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MAMBO YANAYOPENDEKEZWA KUFANYWA USIKU WA LAYLATUL QADR

MAMBO YANAYOPENDEKEZWA KUFANYWA USIKU WA LAYLATUL QADR

Mambo yanayo pendekezwa kufanywa ndani ya Laylatul Qadr
1. Kufanya itikafu
Nayo ni katika kumi lote wala sio usiku wa Lailatu Al-qadr peke yake, kutoka wa A’isha radhi za Allah ziwe juu yake anasema:

[كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَعْتَكِفُ الْعَشْرَ الأَوَاخِرَ مِنْ رَمَضَانَ]      رواه البخاري ومسلم

[Alikuwa Mtume ﷺ akifanya itikafu katika kumi la mwisho wa mwezi wa Ramadhani]         [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

2. Kusimama usiku wake hali yakuamini na kutaraji malipo
Amesema Mtume ﷺ:

[مَنْ قَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ]     رواه البخاري ومسلم

[Atakayesimama usiku wa Lailatu Al-qadr hali ya kuwa na imani na kuridhia, husamehewa yote yaliyotangulia katika madhambi yake]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

3. Kuomba Dua:
Kutoka kwa A’isha Allah awe naye radhi Anasema:

[يا رَسُولَ اللهِ، أرَأيْتَ إنْ عَلِمْتُ أيُّ لَيْلَةٍ لَيْلَةُ الْقَدْرِ، مَا أقُولُ فِيها؟ قَالَ: قُولي: اللَّهُمَّ إنَّكَ عَفُوٌّ كَرِيمٌ تُحِبُّ العَفْوَ فَاعْفُ عَنِّي]     رواه الترمذي

[Nilisema: Ewe Mtume wa Allah, ikiniafikia Lailatu Al-qadr niombe kitu gani? Akasema: Sema: Ewe Mola! Hakika yako wewe ni mwenye kusamehe (madhambi) tena Mkarimu wapenda sana kusamehe, basi nisamehe (makosa yangu)]   [Imepokewa na Tirmidhi.].

4. Kuwaamsha watu wa nymbani kwa ajiliya ibaada
Amepokeya bibi A’isha radhi za Allah ziwe juu yake Amesema:

[كَانَ النبي – صلى الله عليه وسلم – إِذَا دَخَلَ الْعَشْرُ شَدَّ مِئْزَرَهُ، وَأَحْيَا لَيْلَهُ، وَأَيْقَظَ أَهْلَهُ]       رواه البخاري

[Alikuwa Mtume ﷺ likiingia kumi la mwisho akijifunga kibwebwe na akikesha usiku wake na akiamsha wake zake]   [Imepokewa na Bukhari.]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.