AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
4. Mbinu za mashauriano zilifanyika ill Uislamu na Upagani ukutane katikati ya njia. Kwa wapagani na Mushrikina kuacha baadhi ya mambo ambayo walikuwa wakiyafanya, kwa kuzingatia imani yao ya kishirikina, kwa masharti kuwa na Mtume ﷺ naye aache baadhi ya mambo aliyokuwa akiyafanya, kwa kuzingatia imani yake ya Kidini.
وَدُّوا لَوْ تُدْهِنُ فَيُدْهِنُونَ} القلم:9}
[Wanapenda ungalikuwa laini (kwao; ukauiapaka mafuta kwa nyuma ya chupa)] ..[68:9].
Katika upokezi mwingine wa Ibn Jarir na Al- Tabarani, tunafahamishwa kuwa Mushrikina walim-bembeleza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ wakimtaka aabudu miungu yao kwa muda wa mwaka mmoja na wao wamwabudu Mola Wake kwa muda wa mwaka mmoja vile vile. Katika mapokezi mengine ya Abdi bin Humayd, tunafahamishwa kuwa wao walisema kumwambia Mtume ﷺ kama utaikubali miungu yetu na sisi tutamkubali Mungu Wako.(1)
Kupitia njia yake ya upokezi Ibn Ishaq amesema: “Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ alikataa (njia yao ya diplomasia), hali yakuwa anaizunguka Al-Kaaba. ” Al-Aswad bin Al-Muttwalib bin Assad bin Abdi-Uzza na Al-Walid bin Al-Mughirah na Umayya bin Khalaf, na Al- ‘Aswi bin Wail As-Sahamy, walikuwa ni watu waliokuwa na umri mkubwa miongoni mwa Makuraishi, waliwahi kumwambia: “Ewe Muhammad, njoo na tuabudu kile unachokiabudu na wewe uje ukiabudu kile tunachokiabudu, kwa hivyo tutashirikiana sisi na wewe katika jambo hili. Ikiwa yule unayemwabudu ni kheri kuliko kile tunachoabudu sisi tutakuwa tumelichukua fungu letu kwake, na kikiwa kile ambacho tunakiabudiu ni bora kuliko kile unachokiabudu wewe, utakuwa umechukua fungu lako, kutoka katika kile tunachokiabudu sisi. Kuhusiana na rai hii Mwenyezi Mungu ﷻ Akateremsha aya:
{قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ لَا أَعْبُدُ مَا تَعْبُدُونَ وَلَا أَنتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ وَلَا أَنَا عَابِدٌ مَّا عَبَدتُّمْ وَلَا أَنتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ لَكُمْ دِينُكُمْ وَلِيَ دِينِ}
[Sema: Enyi makafiri; Siabudu mnachoabudu; Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu; Wala sitaabudu mnachoabudu;Wala nyinyi hamtaabudu ninayemuabudu; Nyinyi mna dini yenu nami nina Dini yangu.] [109] (2)
Mwenyezi Mungu ﷻ Akawa Ameukata mjadala wao wenye kuchekesha, kwa ufafanuzi huu wenye kukata; na huenda kutofautiana kwa mapokezi haya mbalimbali ni kwa sababu Makureishi walijaribu kufanya majadiliano haya mara kwamara. *
1) Tajhimul Qur’an,Juzuu 6, Uk. 205 na 501.
2) Ibn Hisham, [uzuu 1, Uk. 362.
* Arraheeq Al Makhtum Uk. 143