SOMO LA FIQHI
KUMTANGULIA IMAMU KATIKA SWALA
1. Amri ya Sheria ni kuwa maamuma amfuate imamu wake kwa kufanya kitendo anachofanya imamu wake papo kwa papo, kwa kauli ya Mtume ﷺ:
[إِنَّمَا جُعِلَ الإِمَامُ لِيُؤْتَمَّ بِهِ، فَإِذَا كَبَّرَ فَكَبِّرُوا، وإِذَا سَجَدَ فَاسْجُدُوا] رواه البخاري ومسلم
[Imamu amewekwa afuatwe: akipiga takbri, na nyinyi pigeni takbiri, na akisujudu, na nyinyi sujuduni] [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
2. Imeharamishwa kumtangulia imamu, na Mtume alilitilia hilo makazo mkubwa kwa kusema:
[أما يخشى الذي يرفع رأسه قبل الإمام أن يحول الله رأسه رأس حمار] رواه البخاري ومسلم
[Kwani haogopi ambae anaeinuwa kichwa chake kabla ya imamu, Mwenyezi Mungu amgeuze kichwa chake akifanye kichwa cha punda] [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
3. Mwenye kumtangulia imamu wake kwa kusahau itamlazimu arudi amfuate.
TANBIHI:
Kuswali nyuma ya asiye na Twahara
Swala Haisihi nyuma ya asiye na twahara isipokuwa iwapo hakujulishwa kuwa hana udhu mpaka baada ya kumalizika Swala. Na katika hali hii inasihi swala ya maamuma, na ni juu ya imamu arudie Swala.