KUMGUSA MWANAMKE HUVUNDA UDHUU?
Swali: Mtu anapo kuwa na udhu kisha akamgusa mkewe udhu wake huharibika ?
Jawabu: Mas’ala ya kumgusa mwanamke kuwa ya tangua udhu ama hayatangui ni mas’ala yako na ikhitilafu kubwa kati ya wanachuoni,
A) Kuna wanaosema kuwa udhu unaharibika kwa kumgusa mwanamke kwa namna yoyote ile,na huu ni msimamo wa madhehebu ya Imamu Shafi Allah Amrahamu
B) Kuna wanaosema kuwa kumgusa mwanamke hauvundi udhuu kwa namna yoyote ile sawa iwe kwa kwa matamanio au bila ya matamanio,na huu ni msimamo wa madhehebu ya Imamu Abuu Hanif Mungu amrahamu
C) Na kuna wanaosema kuwa udhuu unaharibika ikiwa utamgusa kwa matamanio,na huu ni msimamo wa madhebu ya Imam Ahmad bin Hanbal Mungu amrahamu.
Na kauli yenye nguvu katika misimamo hii mitatu na yenye kutiliwa nguvu na dalili na hoja ni kauli inaosema kuwa kumgusa mwanamke hakuharibu udhuu, sawa iwe umemgusa kwa matamanio au bila ya matamanio kwa sharti kutotokwa na kitu katika tubu yake.
Na dalili ya Msimamo huu ni hizi zifuatazo.
حديث عائشة رضي الله عنها قالت : [ كنت أنام بين يدي رسول الله صلى الله عليه وسلم ورجلاي في قبلته فإذا سجد غمزني فقبضت رجلي فإذا قام بسطتهما ] رواه البخاري
Hadithi ilio pokelewa na Bibi Aisha Radhi za Mugnu ziwe juu yake asema: [Nilikuwa ni kilala mbele ya Mtume Rehma na amani zimfikie yeye,na miguu yangu nimeinyosha mbele ya kibla chake,akisujudu akinifinya nikiikunja miguu yangu akisimama ni kiinyosha.] [Imepokewa na Bukhary]
Na ushahidi ni kuwa: Mtume ﷺ alimgusa Bibi Aisha Radhi za Allah ziwe juu na yeye yuwaswali na lau ingekuwa kumgusa mwanamke huharibu Udhuu basi Mtume ﷺ angevunda swala kwa kuwa udhuu wake umeharibika.
وعن عائشة رضي الله عنها أن النبي صلى الله عليه وسلم قبل إمرة من نسائه ثم خرج إلى الصلاة ولم يتوضأ [ رواه أبو د وصححه الألباني
Amepokea Bibi Aisha R.A. [Kuwa Mtume ﷺ alimbusu mkewe katika wakeze kisha akatoka kwenda kuswali wala hakutawadha] [Imepokewa na abuu Daud] na kusahihishwa na Al’alabaniy.]
Na Ushaidi ni kuwa mtu anapo mbusu mkewe huwa mara nyingi ni ka wajili ya matamanio, na hapa Mtume ﷺ alimbusu mmoja katika wakeze kisha akaenda kusawali bila ya kutawadha.
Na katika walio rejehesha qauli hii ni Sheikhul- Isalam ibnu taymiyah na katika wanachuoni wakisasa ni Sheikh Ibnu baaz na Sheikh Ibnu Uthaymin Mungu awawelee radhai
Na Allah ndie mjuzi zaidi.