0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

KUINGIA MADINA


AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Baada ya Sala ya Ijumaa, Mtume () aliingia Madina, na kutokea siku hiyo ukaitwa mji wa Yathrib, kuwa ni mji wa Mtume (). Unatamkwa kwa jina la Madina kwa kufupisha; Ilikuwa ni siku ya kihistoria iliyo nzuri kwani majumba na njia zilijaa kishindo kwa sauti za Kumsifu Mwenyezi Mungu () na Kumtakasa. Mabinti wa Ki-Answar waliimba beti zifuatazo kwa furaha na shangwe

طلع الـبدر عليـنا     مـن ثنيـات الوداع

وجب الشكـر عليـنا       مـا دعــــا لله داع

أيها المبعوث فينا    جئت بالأمر المطـاع

 ” llmeangaza mwezi kwetu, kutoka katika lango la maagano

Ni wajibu wetu kushukuru (kwa neema hiya), kwa kuwa tuna mlinganiaji, kwa Mwenyezi Mungu mwenye kulingania,   Ewe ulieletwa kwetu  Umekuja na jambo lenye kufuatwa.”

Answar hawakuwa watu wenye utajiri mkubwa, pamoja na hali hiyo kila mmoja wao alikuwa anatamani Mtume (ﷺ) kufikia kwake. Ikawa Mtume (ﷺ) hapiti katika nyumba yoyote katika nymnba za Answar isipokuwa walikamata hatamu ya ngamia wake, Wakisema; ”Njoo fikia kwetu tuko tayari kukupokea kwani idadi yetu ni kubwa, tuna silaha na tuna uwezo wa kukulinda.”

Mtume (ﷺ) akawa akiwaambia, ”Iachieni njia yake kwani ngamia huyo ameamrishwa”, Ngamia hakusita alienda mpaka alipofika mahali ambapo ndipo ulipo Msikiti wa Mtume (ﷺ) hivi leo, akapiga magoti. Mfume (ﷺ) hakushuka kutoka juu ya ngamia huyo mpaka aliposimama tena na kwenda kidogo, kisha akageuka kidogo na kurejea na kupiga magoti mahali pale pa kwanza, akashuka. Hapo palikuwa ni kwa Banu Najjar, wajomba zake Mtume (ﷺ). Ilikuwa ni katika uwezesho wa Mwenyezi Mungu (ﷻ) kwa ngamia huyo kufanya alivyofanya. Kwani Mwenyezi Mungu (ﷻ) alipenda Mtume (ﷺ) afikie kwa wajomba zake Akikusudia Kuwakirimu kwa kitendo hicho.

Watu wengi walijitokeza na kumuomba Mtumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) ashukie kwao. Lakini ni Abu Ayub Al-Answar ndiye aliyechukua mizigo yake na kuiingiza nymnbani mwake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) akawa anasema; “Mtu anakuwa na mizigo yake (usiichukue).” As’ad bin Zurarah akaja akachukua hatamu ya mnyama wake na akafikia kwake,

Katika upokezi wa Anas (Radhi za Allah ziwe juu yake) kutoka kwa Bukhari, inasemwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alihoji; ”Ni nyumba gani katika nyumba za watu wetu iliyo karibu sana?.” Abu Ayub akasema; “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) hii ni nyumba yangu, na huu ni mlango wangu”, Mtume (ﷺ) akasema, ”Twende ukatuandalie mapumziko.” Mtume (ﷺ) akasema (kumwambia ngamia), ”Simama kwa baraka za M wenyezi Mungu. ” (1)

Baada ya siku chache mke wake Sauda na mabinfi zake wawili, Fatma na Ummu_Kulthum, na Usama bin Zaidi na Ummu Ayman walifika Madina. Pamoja nao katika safari hiyo alikuwa Abdullah bin Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake), familia ya Abubakar pamoja na Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake). Aliyebaki miongoni mwao alikuwa ni Bi Zainab (Radhi za Allah ziwe juu yake), alibaki kwa Abu Al-Assi, hakuweza kutoka mpaka alipohama baada ya vita vya Badri. (2)

Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) ainesema, “Mtume wa Mwenyezi Mmmgu () alipofika ’Madina, masahaba wake, Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) na Bilal (Radhi za Allah ziwe juu yake) walipatwa na maradhi nikaenda nyumbani mwao na kuwasalimia; “U hali gani baba yangu, na unajisikiaje ewe Bilal”; Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) anasema Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) akajibu, ”Kila mtu ni mwenye kupambazukiwa akiwa kati- ya watu wake, na hali ya kuwa kifo ki karibu sana kuliko kamba ya kiatu chake.” (haya maneno alikuwa akipenda kuyatamka Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) wakati akiwa na homa).

Ilikuwa ni kawaida ya Bilal (Radhi za Allah ziwe juu yake) anapoumwa na homa kunyanyua sauti yake na akisema, “Eee, Allah natamani kujuwa ikiwa nitalala usiku mmoja katika jangwa na hali ya kuwa pembeni mwangu kuna mti uitwao Idhkhir, na mti uitwao Jalili, na Ie, iko siku nitayaendea maji ya soko liitwalo Mijamma, na Je, nitapata bahati ya kuyaona majabali yaitwayo Shama na Tufail – ya Makka?

Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema; “Nikamwendea Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) na kumuelezea khabari hiyo”; Akaomba; “Ewe Mala Wangu wa Haki, tufanye tuipende Madina kama tunavyoipenda Makka au zaidi yake, na ifanye Madina kuwa ni mahali pa kupata afya njema, na tia baraka katika pishi yake na kibaba chake na ihamishe homa yake ipeleke huko Juhfa. ” (3)

(Mpaka hapa imekomea sehemu,moja ya maisha ya Mtume (ﷺ) na kukamilika kwa awamu ya da’awa ya Kiislamu ya Makka.)


1)  Sahihil Bukhari, Juzuu 1, Uk. 556. 
2) Zaad Ma’ad, Juzuu 2, Uk. 55. 
3) sahihi Bukhari, Iuzuu 1, Uk. sss-589


Begin typing your search above and press return to search.