ITIKADI YA MASHIA JUU YA UIMAMU
Miongoni mwa itikadi za Mashia ni kuamini Maimamu kumi na mbili, na hili la uimamu ni moja katika nguzo za Uislamu kama wanavyo dai Mashia, na kuwa mtu uislamu wake haukubaliki mpaka aamini maimamu kumi na mbili,na kuwa amali ya mtu haikubaliwi mpaka awe ni mwenye kuamini maimu hawa. Kama yalivyo kuja kwenye Vitabu vyao vya kutegemewa,
Na wamemsingizia Jafar Swadi Mungu amrahamu maneno haya:
إن أول ما يُسأل عنه العبد إذا وقف بين يدي الله ـ جل جلاله ـ عن الصلوات المفروضات، وعن الزكاة المفروضة، وعن الصيام المفروض، وعن الحجّ المفروض، وعن ولايتنا أهل البيت، فإن أقرّ بولايتنا ثمّ مات عليها قُبلت منه صلاته وصومه وزكاته وحجه، وإن لم يقر بولايتنا بين يدي جل جلاله لم يقبل الله منه شيئا من أعماله.
[Hakika jambo la kwanza atakalo ulizwa mja anaposimama mbele ya mola wake mtukufu ataulizwa kuhusu Swala alizofaradhiwa, na ataulizwa kuhusu zaka alizofaradhiwa, na Saumu aliyofaradhiwa na hija aliyofaradhiwa, na ataulizwa kuhusu utawala wa ahlul Bayt, ikiwa ni mwenye kuukubali utawala wetu kisha akawa ni mwenye kufa basi atakubaliwa Swala yake na funga yake na zaka zake na hija yake, na ikiwa hakukubali utawala wetu mbele ya mola alaiyetukuka hatakubaliwa chochote katika matendo yake.] [Aamali Swaduuq: uk 154]
Na wanaitakidi kuwa asiye waamini maimamu kumi na mbili basi huyo si Muislamu bali ni kafiri na ataingia motoni na akae milele humo.
Ameeleza mwanachuoni wao Al Mufiid yakuwa:
إجماع الشيعة الإمامية الاثني عشرية علَى أن من أنكر إمامة أحد من الأئمة وجحد ما أوجبه الله تعالى له من فرض الطاعة فهو كافر ضال مستحق للخلود في النار. (بحار الأنوار 8/ 366، 23/ 390، أوائل المقالات ص44).
[Wameafikiana kwa ujumla wanachuoni wa kishia wanao amini maimamu kumi na mbili yakuwa yoyote yule atakae mkanusha imamu mmoja katika katika maimamu na akapinga aliyowajibishwa na Mwenyezi Mungu mtukufu katika kumtii basi mtu huyo ni kafiri mpotevu anaestahiki kukaa motoni milele] [Biharul Anwaar 8/366,23/390 na kitabu Awaail Al Maqaalat uk 44 ]
Na wanaitakidi kuwa Maimamu wao ni Maasumin wamehifadhiwa na Madhambi kama vile Manabii na wanaitakidi kuwa wanajua ilmul Ghayb mambo yalifichika, na kuwa maimamu wao wanajua siku ya kufa kwao na wao ni bora kuliko manabii wote isipokuwa Mtume Muhammad
Kama yalivyo kuja katika kitabu chao wanachokitegemea sana
Al-Kulayniy katika kitabu ‘Uswuwlul-Kaafiy’: “Kasema Imamu Ja’afar AswSwaadiq:
[Sisi ni hazina ya elimu ya Allaah, sisi ni wafasiri wa amri za Allaah,
Sisi ni watu tuliokingwa na dhambi, imeamrishwa tutiiwe, na imekatazwa
tusiasiwe, Sisi ndio hoja ya Allaah ya wazi kwa viumbe vilivyo chini ya ardhi na mbingu na vilivyo juu ya Ardhi.] [Usuul-ul-Kaafiy cha Al-Kulayniyiy 1/165.]
Itikadi hii ya Mashia juu ya Uimamu ni itakadi potofu kwani yaenda kinyume na Mafunzo ya Qur’ani na Hadithi sahihi za Bwana Mtume ﷺ:
zime kuja aya aya nyingi za kuthibitisha kuwa hakuna ajue Elimu ya Ghayb idipokuwa yeye Mwenyezi Mungu mtukufu Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’ani tukufu:
قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّهُ} النمل:65}
[Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye ya ghaibu isipo kuwa Mwenyezi Mungu.] [Al Naml:65].
Na lakustajabisha ni nguzo hii muhimu kama waanvyo dai Mashia ya kuwa amali za mja hazikubaliwi asipo amini itikadi hii ya Uimamu, kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu asitaje kwenye Qur’ani tukufu wala kushiria kama vile ilivyo kuja Swala, na zaka, na hijja, na Saumu. zimekuja aya zaidi ya moja juu yanguzo hizi tano za Uislamu, lakini hakuna aya hata moja inayoashiria itikadi hii batili Mashia.