ITIKADI YA MASHIA JUU YA MASWAHABA
ITIKADI YA MUISLAMU JUU YA MASWAHABA
Kabla ya kuelezea itakadi ya mashia juu ya Maswahaba kwanza tueleze itikadi ya Muislamu anavyo itakidi juu ya maswahaba wa Bwana Mtume ﷺ.
Sisi waislamu tunaamini kuwa Maswahaba wote ni waadilifu,na wao ndio wanafunzi bora wa Bwana Mtume ﷺ waliitetea dini hii kwa hali na mali, na walijitoa muhanga katika kuineza dini hii ya usilamu Ulimwengu mzima mpaka ukatufikia sisi.Na wao ndio waliokuwa mstari wa mbele katika mambo yote ya kheri.
Mwenyezi Mungu amewachuguwa wawe ndio wenye kusuhubiana na Mtume wake na wawe ni wenye kuisimamia Dini baada ya kufa kwake. Mwenyezi Mungu ametaja sifa zao katika Qur’ani tukufu pale alipo sema:
مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّهِ وَرِضْوَانًا ۖ سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ ۚ ذَٰلِكَ مَثَلُهُمْ فِي التَّوْرَاةِ ۚ وَمَثَلُهُمْ فِي الْإِنجِيلِ كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْأَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ ۗ وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنْهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا الفتح:29
[Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea ulio toa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Mwenyezi Mungu amewaahidi walio amini na wakatenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa.] [Al Fathi:29]
Na Mwenyezi Mungu amewawelea Radhi, na alowelewa radhi na mungu hawi mbaya Maisha yote.Mwenyezi Mungu anasema:
وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ التوبة:100
[Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.] [Al Tawba:100]
Na Mwenyezi Mungu ataja sifa za waumini ni kuwa wanawaombea msamaha walio watangulia kabla yao,asema Mwenyezi Mungu mtukfu:
وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ} الحشر:10}
[Na walio kuja baada yao wanasema: Mola wetu Mlezi! Tughufirie sisi na ndugu zetu walio tutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walio amini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu.] [Al Hashri:10]
hii ndio itakidi ya Muislmu juu ya Maswahaba wa bwana mtume na wanaimani kuwa wao ndio watu bora katika Umma huu.
MASHIA WANAITIKIDI VIPI ?
Imejengeka itikadi ya Raafidwah juu ya kuwatukana na kuwakufurisha Maswahaba wa Mtume ﷺ Rahma na amani zishuke juu yao.
روى الكليني عن أبي جعفر رحمه الله تعالى قوله : “كان الناس أهل ردة بعد النبي صلى الله عليه وآله وسلم إلا ثلاثة . فقلت : من الثلاثة ؟ فقال : المقداد ابن الأسود ، وأبو ذر الغفاري ، وسلمان الفارسي العياشي: 1/223 الكافي: 8/245
Ametaja Al-Kulayiniy kutoka kwa Ja’afar “Waliritadi watu wote baada ya Mtume ﷺ isipokuwa watu watatu; Nikasema: Ni kina nani hao watatu? Akasema ni Miqdaad bin Aswad, na Abu Dhariy Al-Ghifaariy, na Salmaan Al-Faarisiy.]” [Al-Ayaashi 1/223] Al-Kaafiy 8/2245
عن أبي علي الخراساني عن مولى لعلي بن الحسين عليه السلام قال: كنت معه عليه السلام في بعض خلواته فقلت: إن لي عليك حقا ألا تخبرني عن هذين الرجلين: عن أبي بكر وعمر؟ فقال: كافران كافر من أحبهما
Kutoka kwa Aliy bin Al-Husayn kasema: [Nilikuwa naye (Alayhis-Salaam) katika baadhi ya sehemu alizokuwa akijitenga, nikasema kumwambia: Hakika mimi ninashakia baadhi ya haki kwako, naomba nieleze kuhusu watu hawa wawili, Abu Bakr na ´Umar, Akasema: Ni makafiri na kila mwenye kuwapenda ni kafiri.]
Pia isitoshe kuwakufurisha,bali wanawalani na kuwapiza na kuweka dua Makhsusi inayojulikana Dua ya masanamu wa kiquraish yamekuja haya katika kitabu chao [“Iqtidhaa siratul Mustaqim Mukhalafatul as’haabul jahim 1/446]
للهم العن صنمي قريش وجبتيها وطا غو تيهما وإفكيها وا بنتيهااللذين خالفا أمرك،وأنكرا وحيك،وجحدا نعامك وعصيا رسولك،وقلبا دينك، وحرفا كتابك وأحبا أعدائك وجحدا آلاءك وعطلاأحكامك …. إلى آخره
Ee Mwenyezi Mungu walaani masanamu wawili wa ki-Quraysh, na Matwaaghuti wao, na wazushi wao na mabinti wao ambao walikhalifu mamrisho yako na wakakanyusha wahyi wako na kuzikanyusha neema zako na wakamuasi Mtume wako na wakageuza Dini yako na Kugeuza kitabu chako na wakawapenda madui zako na kukanyusha ukubwa wako na kutumbiliambali hukmu zako …
Na Dua hii mashia wameitilia umuhumu sana na wameisherehesha katika vitabu 10
imepokewa toka kwa Abu Hamzah Athumaliy kwamba alimuuliza ´Aliy bin Al-Husayn kuhusu Abu Bakr, Akasema; “Nikafiri na kila atakaemuunga mkono pia ni kafiri. [Bihaarul-Anwaar cha Al-Majlisiy 69/137-138.]
hizi ni baadi ya dondoo kwenye vitabu vyao na lau tungetaka kunukuu walio yandika kwenye vitabu vyao vyote makala yangekuwa marefu sana lakini yatosha haya tulio yanukuu,na kwa ulimwengu waleo ulimwengu wa utanda wazi yamedhihiri mengi kwa sauti na kwa Vedio za Mashekhe wao wakithibitisha itikadi hii mbya juu ya Maswaha wa Bwana Mtume ﷺ.
Msikilize huyu Sheikh wao asema wazi wazi bila yakuficha kuwa jibwa wa Ariel Sharon ni bora kuliko abuu Bakar na Omar, je kuna ukafiri zaidi ya hilo.na Baado kuna walio danganyika wakidai kuwa ni urongo wasingiziwa Mashia