NI IPI ITIKADI YA “TUQYA” KWA MASHIA ?
Amesema mmoja wa Wanavyuoni wao wa zama hizi kuwa:
“Taqiyyah ni kitendo cha mtu kusema au kufanya kinyume na vile anavyoitakidi, kwa lengo la kujikinga na madhara yeye au mali yake au kulinda utu na heshima yake.”(1)
Na wanadai kwamba Mtume (ﷺ) alifanya Taqiyyah wakati alipokufa kiongozi wa wanafiki ´Abdullaah bin Ubay bin Saluwl, pindi alipokuja kumswalia, kisha ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhu) akamwambia Mtume (ﷺ). “Hivi Allaah si kakukataza kumswalia mtu huyu mnafiki?, Mtume (ﷺ) akamwambia wewe unajua ni nini nimesema? Nimesema: “Ee Mola wangu mjaze ndani yake moto, na ulijaze kaburi lake moto, na umuingize motoni.”(2)
Hebu tazama ndugu yangu Muislamu vipi wanamzulia na kumnasibisha Mtume (ﷺ) na uongo?!
Hivi inaingia akilini kwamba Maswahaba wa Mtume (ﷺ) wanamtakia Rahma na Mtume (ﷺ) akimlaani?!
Na amenukuu Al-Kulayniy katika ‘Uswuwlul-Kaafiy’: “Kasema Abu ´Abdillaah: “Ewe Abu ´Umar hakika asilimia tisa ya dini ipo katika taqiyyah, na hana dini asiyekuwa na Taqiyyah, na Taqiyyah inaingia katika kila kitu isipokuwa katika pombe na kupangusa juu ya khufu.”
Na amenukuu vilevile Al-Kulayniy toka kwa Abu ´Abdillaah kwamba amesema: “Icheni dini yenu, na ikingeni kwa Taqiyyah, kwa hakika hana imani asiyekuwa na Taqiyyah.”(3)
Bali imefikia hali kwa Raafidhwah wanajuzisha kuapa kwa asiyekuwa Allaah kwa mujibu wa Taqiyyah!!
Ameyaeleza hayo Al-Huru Al-‘Aamiliy katika kitabu chake ‘Wasaailu AshShi’ah’ kuwa imepokewa kutoka kwa Abu Bukayr, kutoka kwa Zuraarah kutoka kwa Abu Ja’afar (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema:
“Nilisema kumwambia Abu Ja’afar: “Hakika sisi tunapita kwa watu wanatutaka tuape juu ya mali zetu na ilihali tumeshakwishazitolea Zakaah, akasema (Abu Ja’afar): Ewe Zuraarah pindi utakapochelea hilo basi wewe apa kwa vyovyote vile watakavyotaka, nikamuuliza: Hata kuapa kwa talaka? Akasema kwa chochote watakachotaka.”
Na imepokewa toka kwa Suma’ah toka kwa Abu ´Abdillaah amesema:
“Pindi mtu atakapoapa kwa Taqiyyah hakuna tatizo maadam kalazimishwa, na kalazimika kufanya hivyo.”(4)
Raafidhwah wanaitakidi kuwa Taqiyyah ni faradhi ambayo madhehebu yao hayasimami bila ya Taqiyyah, na wanaitumia hasa hasa katika mazingira magumu, hivyo inatakiwa ndugu Muislamu utahadhari sana na hawa Raafidhwah. *
1) Ash-Shi’at fiyl Miyzaan, cha Muhammad Jawaad Mughniyah uk. 47.
2) Furuw’ul-Kaafiy, Kitaabul Janaaiz uk. 188.
3) Uswuwlul-Kaafiy cha Al-Kulayniy uk. 482-483.
4) Wasaail Ash-Shi’ah cha Al-Hurru Al-‘Aamiliy 16/136-137.
* MIONGONI MWA ITIKADI ZA MASHIA ‘Abdullaah Bin Muhammad As- Salafiy Uk / 22