SOMO LA FIQHI
Suali: Nipi hukumu ya swala tano?
Jawabu: Swala tano ni wajibu kwa kila Muislamu, kulingana na mafundisho ya Qur’ani, na Sunna na Ijmaa ya wanachuoini (umoja wa wanavyuoni):
1. katika Qur’ani:
Anasema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
{وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَارْكَعُوا مَعَ الرَّاكِعِينَ} البقرة:43
[Na simamisheni Swala na toeni Zaka na rukuuni pamoja na wenye kurukuu] [Al-Baqara: 43].
Na Amesema tena katika aya nyingine:
{إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا} النساء:103
[Kwani hakika Sala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu] [Al-Nnisaai:103]
2. Na katika Sunna:
بني الإسلام على خمس : شهادة أن لا إله إلا الله ، وأن محمدا رسول الله ، وإقام الصلاة ، وإيتاء الزكاة ، وحج البيت ، وصوم رمضان رواه البخاري ومسلم
Amesema ﷺ:[Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano: kushuhudia kuwa hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mja Wake na mtume wake, na kusimamisha Swala, nakutoa Zaka, nakuhiji Alkaba na kufunga mwezi wa Ramadhani] [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
Na imepokewa kutoka kwa Twalhah bin ‘Ubeidillah kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume ﷺ kuhusu Uislamu, akasema ﷺ:
[خمسُ صلواتٍ في اليوم واللَّيلة]، فقال هل عليَّ غيرها؟ قال: [لا، إلاَّ أن تَطوَّع]
[Ni Swala tano mchana na usiku. Akasema: “Je, kuna nyingine zinazonilazimu sizizokuwa hizo?” Akasema: La, isipokuwa ukijitolea] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
3. Umoja wa wanavyuoni:
Umma kwa umoja wao wamekubaliana juu ya uwajibu wa Swala tano kipindi cha mchana na usiku,na kuwafikiana bila ya khitilafu yoyote kwamba swala ni mojawapo ya nguzo za Uislamu.
SWALA INAMLAZIMU NANI?
Swala inamlazimu kila Muislamu, aliyebaleghe, mwenye akili, awe mwanamume au mwanamke.