Suali :
Ni ipi hukumu ya kuweka mlio wa simu kwa sauti ya kisomo cha Qur’an ??
Jawabu :
Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu ,Na rehema na amani zimfikie Bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Haijuzu kwa Muislamu kuweka sauti ya mlio wa Simu kwa kutumia sauti ya usomaji wa Qur’ani Tukufu. Kwa sababu hili linaiweka wazi Qur’ani kwa yale yasiyofaa, kama vile kukatisha kisomo, kutozingatia maana yake, na kuitumia kwa malengo yasiyokuwa yale ambayo iliteremshwa kwayo, kama vile kutafakari, kuzingatia na kuitendea kazi
Na imekuja katika maamuzi yaliyopitishwa na kituo cha Fiqhi cha kiislamu ambacho kipo chini ya Taasisi ya Rabitwa tul Alamil Islamy ama (World Muslim League) nambari (107) (19/1) yafwatayo : “Hairuhusiwi kutumia aya za Qur’ani Tukufu kuweka mzinduo au (Alarm) au kumsubirisha mtu kwa kutumia Aya hizo za Qur’an katika simu za mkononi na yaliyo katika hukmu ya simu za mkononi. Na hilo ni kutokana na kwamba kuitumia Qur’an kwa namna hii kunaiweka Qur’an katika hali ya kudharaulika kwa kukata kisomo na kuipuuza , na kwa sababu pia huenda Aya za Qur’an zikasomwa katika sehemu zisizofaa ”
Na Allah ndie mjuzi zaidi