HUKMU YA KUVAA NIQAAB KATIKA IBADA YA UMRA NA HAJJI
SWALI: Nini hukumu ya mwanamke alie hirimia umra kisha akavaa Niqaab na kufinika uso wake?
JAWABU: Mwanamke akihirimia ibada ya umra au hajji huwa haifai kufinika uso wake kwa kuvaa niqaab au kuvaa soksi za mikono,kama ilivyo kuja katika hadithi ya Mtume kuhusu Mwanamke alie hirimia
عن ابن عمر رضي الله عنهما أن رسول صلى الله عليه وسلم قال : ” لاتنتقب المرأة المحرمة ولا تلبس القفازين ” . رواه البخاري
Kutoka kwa Ibnu Umar radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kwamba Mtume amesema: [Asivae niqaabu mwanamke alie kwenye ihramu na asivae soksi za mikono] [imepokewa na Bukhari]
Lakini ikiwa atafunika uso wake kwa kutojua hukmu yake au kwa kusahau atakuwa hawajibiki na kitu chochote ,lakini kama alikuwa anajua basi atakuwa na khiyari kufanya moja katika mambo matatu,ima afunge siku tatu,au alishe masikini sita kila maskini nusu ya pishi,au achinje mbuzi na aigawe nyama yake kwa masikini wa mji wa makkah.
Na Mwenyezi Mungu ndie mjuzi zaidi.