Dkt. Gary Miller
Huyu ni mwanahisabati na mwanatheolojia wa kutokea Canada. Alikuwa akijitolea kufanya kazi za kimishenari za Kikristo katika maisha yake lakini akaja kugundua mambo mengi yenye mashaka katika Biblia. Mwaka 1978 alianza kuisoma Qur’an akitaraji atakutana na mchanganyiko wa ukweli na uongo pia. Aligundua kwa mshangao kuwa ujumbe uliobebwa katika kitabu hiki cha Qur’an unaendana vilivyo na ule ujumbe uliopatikana katika Biblia baada ya kuchujwa. Akawa Muislamu na tangia hapo amekuwa ni mwenye kufanya mihadhara mbali mbali ya umma kuhusu Uislamu akitokea katika redio na televisheni pia. Vile vile ni mtunzi na wa makala nyingi za kiislamu. Akiwa na mtaalamu wa hisabati katika Chuo Kikuu cha Toronto, aghalabu amekuwa ni mwenye kuchambua jambo kwa utaalamu wa hali ya juu. Na hivyo, Gary Miller akafanya uchanganuzi wake kwa aya za Qur’an na matokeo yakawa ni kujisalimisha kwa mtunzi wake. Hii ni moja ya aya za kitabu hiko:
[Hebu hawaizingatii hii Qur’ani? Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake khitilafu nyingi] [Q 4:82]
Akiongelea aya hii, Dkt. Miller anasema: “Moja ya kanuni kubwa ya kisayansi ni ile kanuni ya kutafuta makosa, au kuangalia dosari katika nadharia mbalimbali mpaka itapowekwa sawa (Falsification Test). Cha kushangaza kitabu hiki cha Qur’an tukufu kinawauliza Waislamu na wasio Waislamu wajaribu kutafuta makosa ndani yake na kuwahahkikishia kuwa hawatapata hitilafu hata kidogo…Hakuna mwandishi yeyote hapa duniani mwenye ujasiri wa kuandika kitabu na kusema hakina makosa, lakini Qur’an imediriki kusema haina makosa na inakushajihisha ujaribu kutafuta kama utapata hata moja.”
Mwaka 1977, Profesa Miller (akiwa bado Mkristo) alifanya dahalo wa kidini na mwanachuoni mashuhuri wa kiislamu A h m e d Deedat. Na i l i p o t i m u 1978, baada ya kupokea dalili nyingi zaidi zioneshazo ukweli wa Ui s l amu, Professa Miller aliamua kuwa Muislamu na kuchukua jina la Abdul-Ahad likimaanisha ‘Mja wa Aliye Mmoja (yaani mja wa Mungu)’. Amefanya kazi kwa miaka kadhaa katika Chuo Kikuu cha Mafuta na Madini,Saudi Arabia na kujitolea maisha yake katika kuuhubiri Uislamu kupitia vipindi vya televisheni na mihadhara ya wazi. Gary Miller ametunga makala mbali mbali kuhusu masuala ya dini.**
** Hii ilikuwa ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho“Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” Kwa usomaji wa ziada tembelea www.extremelysmart.org au www.facebook.com/muerevumno “**