JE YESU MWANA WA MARYAM ALIKUFA MSALABANI?
Kifo ni jambo nzito mno na halifichiki, wala hutakiwi ujaribu kutoa maelezo ili kudhibitisha eti mungu wako alikufa, kwanza ni aibu na kufru kudai eti aliyekuumba aweza kuuwawa na viumbe vyake, na ikiwa hilo litatokea, basi fahamu moja kwa moja WEWE humuabudu Mola, bali uko katika ibaada ya masanamu au mashetani. Jambo la pili huwezi kutumia maandiko ya Paulo aliyeazimu kwenda kinyume na Nabii Yesu[as] mwana wa maryam, kuwa neon la msalaba kwa wanaopotea ni upuuzi.
Hapa bwana watetea kitu Fulani na sina shaka ni mkate wako wakila siku.
Qur’aan imesema kuwa kila nafsi itaonja mauti, na kuwa baadhi ya Manabii waliotimilizwa sehemu mbali mbali walipata mateso na wengine wakawa ni wenye kuuwawa. Kwa ayah ii kamwe siyo dalili ya kufa kwa Nabii Issa [Alayhi salaam] mwana wa maryam, bali ni dalili kuwa Bwana Fondo analenga tena kutumia aya zake Allah mtukufu kijanja, na hatuna shaka haya yatamrudi kama yalivyo warudi wale waliofanya azma ya kupigana na Mola na wakashindwa vibaya.
Katika Qur’ani 3:55, Mwenyezi Mungu mtukufu anatupa habari namna wayahood walivyopanga njama za kumwangamiza Yesu, lakini Mola akazipindua hila zao, akamwambia nitakutimizia muda wako wa kuishi, HAWATAKUUA hawa maadui, na nitakuleta kwangu NA NITAKUTAKASA. Waweza kutumia lugha uitakayo, lakini ukweli utabakia, pili neno nitakufisha kilugha katu halina maana ya kufariki dunia, na Yesu [as] asingelisema ‘ waache wafu wazike wafu wao ‘ lakini najua hiyo kwako ni fikra ngumu.
Qur’ani imetoa msimamo mmoja kuwa Nabii Issa Yesu [Alayhi salaam] hakufa kamwe msalabani kama wanavyodai wenyekujitafutia katika Qur’ani 4:156-158.
[Na pia kwa kufuru zao na kumsingizia kwao Maryamu uwongo mkubwa.Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu – nao hawakumuuwa wala hawakumsalibu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo.
Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakiniBali Mwenyezi Mungu alim- tukuza kwake, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.]
Wayahood walidhani Nabii atakae tumwa kwao atawaongoza katika vita dhidi ya warumi waliokuwa wakiwatawala zama hizo, lakini kinyume chake akawa mpole na kulipa ushuru kwa warumi, hili liliwafanya wayahoodi waanzishe fitina nyingine ambayo ipo hata leo kuwa Mama Maryam alifanya uchafu ili azaliwe Yesu [Alayhi salaam] Hii ndio sababu yao kupanga njama za kumuangamiza.
Biblia imeandikwa na hao waandishi kuwa kila mwenye madhambi makubwa kama ubakaji, mauaji yasiyo ya haki, hukumu yao ni kuuwawa kwa kusulubishwa, katika Torati 21:22, vipi huyu unaye muita mungu wako afe kifo cha fedheha?, ikiwa Yesu [as] hakutenda dhambi niwazi kuwa hakufa msalabani, na kama tulivyo bainisha, kwanini adhulumiwe?
Wako wakristu wengi wasio jua kuwa msalaba ni chombo kitesi, na misalaba ilikuweko miaka mingi kabla hajazaliwa Yesu [as] mwana wa maryam, na katika Tourati aliyo pewa Nabii Musa [Alayhi salaam] kuwa kila aliyeangikwa msalabani amepata laana yake Allah [swt], nasi waislam katu hatukubali Nabii Issa [Alayhi salaam] aliingizwa katika laana kama anavyodai bwana Fondo na wote wenye fikra kama yake, lakini vipi afe kifo hicho cha laana hali yeye ndiye mungu kwa wakristu!. Kwa nini sisi tujiingize katika hali ya kutatanisha na kujaribu kutoa sababu zetu wenyewe zisizo kuwa na msingi wowote.
Ndugu wasomaji ni Qurani pekee iliyo simama kidete katika kufahamisha ukweli ambao umefichwa kwa miaka mingi kuwa Yesu [as] hakufikishwa msalabani, na kuwa msimamo huu umebakia katika hali hiyo hiyo kwa takriba miaka 1438, kinyume na vitabu vingine ambavy hubadilishwa kila uchao, na kwake kudai kuwa Biblia yote ni maandiko yake matakatifu ni uwongo wa hali ya juu kwa mtu huyu anaye tafuta umaarufu, na makasisi ishirini na tisa kati ya makasisi thelathini na moja wa Uingereza wamekiri kwamba Yesu [as] kweli aliishi humu duniani, lakini kwamba alisulubiwa ni uwongo wa kujitafutia maslahi. Mgongano ulioko kwenye Biblia ni wakutishia, mfano alivaa nguo rangi gani nyekundu au zambarau, alisulubiwa saa tatu asubuhi au saa tisa?
Kando na migongano tuliyo nukuu hapo, bado utaona utata wa wale waliokwenda kaburini kungali asubuhi ili ‘kuupaka’ mwili wake mafuta walikuwa wangapi, mfano:-
1. Mathayo 28:1-2–wanawake wawili [2] tu ndiyo walio kwenda kaburini, Mariam Magdalene na mariam wa pili.
2. Marko 16:1-3–waliokwenda kaburini ni Mariam Magdalene, Mariam mamaye Yakobo, na Salome [3]
3. Luka 24:1, 10—waliokwenda kaburini alfajiri ni wengi tu sana, mariam Magdalene, na Yoana, mariam mamaye Yakobo, na wale wanawake wengine!
4. Yohana 20:1—Aliyekwenda kaburini ni mmoja tu naye ni Mariam Magdalene.
Nani awezaye kuamini mambo haya yasiyoelekea, lipi la kuaminika katika vitabu hivi vinne visivyoelekea, kasha tudai kutafuta mwongozo wa kisawa. Jambo linguine la ajabu ni kuwa kwa taratibu na mila za wayahood wanawake katu hawaendi makaburini, wala haijatokea kuwa maiti aliye zikwa siku tatu aweza fukuliwa tena ili maiti apakwe mafuta, lakini kwenye Biblia ambayo Fondo angependa tuiamini imeandikwa hayo ya yakuchekesha.
Katika Mathayo 27:62-66, Nabii Yesu [as] mwana wa Maryam ameitwa mjanja!, na juu ya yote wakasema kuna uwongo ule mwisho utapita ule kwanza, ajabu hata leo wasomi katika ukristu hawataki kueleza maneno hayo. Mara nyingi utaona kuwa ndugu Fondo anadumu katika kutoa maelezo yake ili kujaribu kufidia pale anapodhania kuwa kuwa anavyofikiri, amekuwa mhariri wa Mwenyezi Mungu!
Tangu jadi kuna madhambi ambayo waja wanatoa kafara kwa kuchinja mnyama ima kondoo, ngombe, mbuzi au ngamia, na sio lengo kuwa mnyama mmoja asafishe madhambi ya watu wote kama anavyofikiri Bwana Fondo na angependa sote tuwe kama alivyo jambo ambalo haliwezekani kamwe.
IMETAYARISHWA NA :
ADAM AMBETSA
MWEMBE TAYARI TABLIGH GROUP
MOBILE NO. 0723 17 41 54
MOMBASA, KENYA.