AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Wakati wa msimu wa Hijja katika mwaka wa kumi na tatu wa Utume sawasawa na mwezi wa Juni mwaka 622 C.E. walihudhuria Waislamu zaidi ya sabini kutoka Yathrib kwa madhumuni ya kutekeleza matendo ya Hijja. Walikuja mahujaji wa kutoka huko wakichanganyika na Mushirikina. Waislamu hawa walikuwa wameulizana kati yao (hali ya kuwa wao bado wako “Yathrib au walipokuwa njiani), ‘Mpaka. lini tutamwacha Mjumbé wa Mwenyezi‘ Mungu (ﷺ) akizunguka zunguka na kufukuzwa katika majabali ya Makka akiwaogopa Mushiriki.na?.’ Walipofika Makka walifanya mawasiliano ya siri kati yao na Mtume (ﷺ) yaliyowafanya kukubaliana kuwa makundi yao mawili yakutane katikati ya masiku ya Tashriq, katika bonde ambalo liko mbele ya Aqabah mahali ambapo kipo kikuta cha mwanzo cha Mina na kuwa kukutana huko kufanyike kwa siri kubwa wakati wa kiza cha usiku. Na tumwache mmoja wa viongozi wa Answari atusimulie kuhusu mkutano huu wa kihistoria ambao uliyageuza mapito ya masiku katika mapambano ya Upagani na Uislamu;
Ka’ab bin Malik Al Answary (Radhi za Allah ziwe juu yao) alisema; ”Tulitoka tukielekea kwenye Hijja, na tulikuwa tumemuahidi Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) kuwa tutakutana naye pahala tulipoahidiana, katikati ya masiku ya Tashriq na ulikuwa ni usiku tulioahidiana na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ). Pamoja nasi alikuwepo Abdullah bin Amri bin Hizam. Bwana miongoni mwa mabwana zetu na Mtukufu miongoni mwa Watukufu wetu, tulimchukua pamoja nasi wakati wote tulikuwa tukiwaficha jamaa zétu waliokuwa bado ni Mushirikina jambo Tukazungumza nae; “Ewe Aba Jabir kwa hakika wewe ni Bwana miongoni mwa mabwana zetu na ni Mtukufu miongoni mwa Watukufu wetu, kwa hakika sisi tunakushauri kuwa ni bora ukaachana na itikadi uliyonayo ili usije kuwa kuni za moto wa Jahannam.
Baada ya hapo tukamlingania aufate Uislamu na tukamweleza kuhusu ahadi tuliyonayo ya kukutana na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) huko Aqaba, alisilimu na akahudhuria pamoja nasi Aqaba akiwa kiongozi.” Kaab alisema: ”Usiku ule tulilala pamoja na jamaa zetu katika kambi zetu mpaka ilipopita theluthi ya usiku, tulitoka katika kambi zetu ili kwenda kutimiza ahadi tuliyowekeana na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ), tulichomoka kama ndege wadogo, kwa kujificha mpaka tukakusanyika katika bonde mbele ya Aqabah kama tulivyokubaliana, Tukiwa watu sabini na watatu wanaume na wanawake wawili katika wake zetu. Nao ni Sibah bint Ka’ab na Ummu ’Amaarah katika Banu Maazin bin Najjar, na Asmaa bint ’Amru Ummu Manii katika Banu Salma. Tukakusanyika katika bonde tukimsubiri Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) mpaka alipofika akiwa pémoja na ammi yake ‘Abbas bin Abdl Muttwalib na hali ya kuwa bado yu katika dini ya watu wake – alifanya hivyo kwa sababu alipenda kuhudhuria jambo la mtoto wa ndugu yake, alimthibitisha na alikuwa mtu wa kwanza kuzungumzafifii.