AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Mtume (ﷺ) Akiwa Taif:
Katika mwezi wa Shawwal mnamo mwaka wa kumi wa Utume (Mwishoni mwa mwezi wa Juni mwaka wa 619 C.E.), Mtume (ﷺ) alitoka kuelekea Taif. Mji wa Taif uko mbali na mji wa Makkah kwa kiasi cha maili sitini (60), alikwenda huko Taif kwa miguu, alikwenda na kurudi akiwa pamoja na kijana wake Zaid bin Haritha. Kila alipolipita kabila lolote njiani alisimama na kulilingania kwenye kuufuata Uislamu. Lakini kwa bahati mbaya hakuna kabila hata moja lililoitika Da’wa yake ya kuukubali Uislamu. (1)
Alipofika Taif aliwakusudia ndugu watatu katika viongozi wa kabila la Thaqif, nao ni Abdil Yali, Masoud, na Habba – watoto wa ’Amru bin ’Umayr Al-Thaqafy. Alifikia kwao na akawalingania kwa Mwenyezi Mungu (ﷻ) na kwenye kuunusuru Uislamu. Mmoja wao akasema: “Nitazichana nguo za Al-Ka’abah ikiwa kweli umetumwa na Mwenyezi Mungu…”. Akasema mwengine, “Hivi Mwenyezi Mungu hakupata mtu mwengine asiyekuwa wewe?.” Na akasema ndugu wa tatu: ”Naapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu, sitakusemesha milele ukiwa ni Mtume. Kwa hakika una hatari kubwa sana kuliko mimi kukusemesha maneno na kwa hakika iwapo utakuwa mwongo kwa Mwenyezi Mungu haitakikani kukusemesha.”
Mtume (ﷺ) akasimama na kuondoka na kuwaambia; ”Chochote mtakachofanya juu yangu si neno, lakini nifichieni khabari zangu.”
Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alifanya kazi ya kufikisha ujumbe kwa watu wa Taif kwa muda wa siku kumi, hakumwacha yeyote katika watukufu wao isipokuwa alimwendea na kusema naye. Wote hawakufurahishwa na kumwambia, ”Toka katika mji wetu.” Mtume (ﷺ) akaamua kuondoka na wakati anaondoka wakawashakizia wajinga na watumwa wao, hali ya kuwa wanamtukana na kumpigia kelele, mpaka wakamkusanyikia watu, wakamsimamia watu waliojipanga katika misitari miwili na kuanza kumpiga kwa mawe huku wakimtukana kwa maneno ya kipumbavu. Walimpiga kwa mawe miguuni mpaka vikaroa damu viatu vyake.
Wakati wote huo Zaid bin Haritha (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikuwa akijitahidi kumkinga dhidi ya mawe yale kiasi cha kupasuliwa kichwani. Hawakuacha kumuandama wajinga mpaka alipoegemea katika bustani ya watoto wawili wa Rabia, ’Utba na Shaiba. Wakiwa kiasi cha maili tatu kutoka Tail, alipokimbilia kwenye bustani hiyo walimwacha na kurejea.
Mtume (ﷺ) akaenda kwenye tawi la mzabibu na kukaa chini ya kivuli chake ameegemea ukuta. Alitulizana na kuomba kwa yale maombi yanayojulikana, maombi ambayo yanafahamisha jinsi moyo wake ulivyojaa huzuni kutokana na yale ambayo ameyapata katika taabu na matatizo kwa kuhuzunika zaidi kwa kuwa hakuaminiwa hata na mtu mmoja miongoni mwa watu Wale. Akaomba:
اللهم إليك أشكو ضعف قوتي ، وقلة حيلتي ، وهواني على الناس ، أرحم الراحمين ، أنت أرحم الراحمين ، إلى من تكلني إلى عدو يتجهمني ، أو إلى قريب ملكته أمري ، إن لم تكن غضبان علي فلا أبالي ، غير أن عافيتك أوسع لي ، أعوذ بنور وجهك الذي أشرقت له الظلمات ، وصلح عليه أمر الدنيا والآخرة ، أن تنزل بي غضبك ، أو تحل علي سخطك ، لك العتبى حتى ترضى ، ولا حول ولا قوة إلا بك
“Ewe Mola wangu wa Haki ninaushitaki Kwako unyonge wa nguvu zangu na uchache wa mbinu zangu na unyonge wangu kwa watu, Ewe Mrehemevu zaidi wa wenye kurehemu. Wewe ni Bwana wa wenye kudhoofishwa na Wewe Ndiye Bwana Wangu ni kwa nani unanitegemeza? Ni kwa aliye mbali atakayenishambulia? Au kwa adui ambaye umemmilikisha mambo yangu ? Pakitoka kwako machukivu juu yangu, sijali jambo lolote isipokuwa Msamaha Wako ndiyo mpana zaidi kwangu. Ninataka hifadhi kwa Nuru ya Dhati Yako Ambayo imeondoa kwayo giza, na yametengenea juu yake mambo ya dunia, na bora kuliko kunishukia Adhabu Zako, ni Yako radhi mpaka uridhie na hapana kukengeuka nu kuepukana na maovu na hapana nguvu ya kufanya mema isipokuwa kwa Msaada Wako.”
Watoto wawili wa Rabia walipomwona walisisimka kwa kumhurumia, wakamwita mtumishi wao aliyekuwa Mkristo, anayeitwa Addas, wakamwambia: ’Chukua zabibu hizi na umpelekee mtu yule. Alipoziweka mbele ya Mtume (ﷺ), Mtume (ﷺ) aliunyoosha mkono wake kwenye zabibu huku akisema: ”Kwa Iina la Mwenyezi Mungu ” kisha akala. Addasi akasema, “Kwa hakika maneno haya huwa hayasemwi na watu wa miji hii”, Mtume (ﷺ) akamwuliza yule kijana, “Umetoka mji gani? Na ni ipi dini yako?’ Yule kijana akajibu, “Mimi ni Mkristo katika watu wa ”Ninawa”‘. Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) akamwambia, ”Unatoku katika kijiji cha mtu mwema, Yunus bin Matta”, yule kijana akahoji, ”Kitu gani kimekujulisha kuhusu Yunus bin Matta?” Mtume (ﷺ) akajibu, ”Huyo ni ndugu yangu, alikuwa Mtume na mimi ni Mtume.” Baada ya kusikia maneno hayo Addasi akasimama na kumbusu Mtume (ﷺ) mikono yake na miguu yake, akivibusu viungo hivyo, watoto wa Rabia wakashangazwa sana na mmoja akamwambia mwingine, ama kwa hakika mtumishi wako ameharibiwa. Addasi aliporudi walimwambia; ”Umetustaajabisha, ni jambo gani lile ulilolifanya?’ Naye akawajibu kwa kusema; “Enyi mabwana zangu, hakuma kitu chochote kilicho bora katika dunia hii kuliko mtu huyu, kwani amenieleza mambo ambayo hayajui mtu isipokuwa Mtume.” Wakamwambia, ”Tunakushangaa ewe Addasi, mtu huyu asije akakupotosha na kukutoa katika dini yako, dini yako ni bora kuliko dini yake.”
Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) akarejea katika njia ya Makka baada ya kutoka katika ile bustani hali ya kuwa ni mwenye huzuni, aliyevunjika moyo. Alipofika Qarni nl-Mzmazil, Mwenyezi Mungu (ﷻ) Alimteremshia Jibril (Alayhi Salam) akiwa pamoja na Malakul Jibal (Malaika wa majabali) akimshauri kuyafunika majabali mawili juu ya watu wa Makka. Bukhari amepokea katika ufafanuzi wa kisa hiki kwa njia ya upokezi kutoka kwa Urwa bin Al-Zubair (Radhi za Allah ziwe juu yake) kuwa Aisha (Radhi za Allah ziwe juua yake.) alimzungumzia kuwa yeye aliwahi kumwuliza Mtume (ﷺ), ” Je, imewahi kukutokea siku ambayo ilikuwa ni siku ngumu sana kwako kuliko siku ya Uhud?’ Akujibiwa, ”Nilikutana kutoka kwa jamaa zako na yale ambayo nilikutana nayo kutoka kwao siku ya Al-Aqabah, kwani niliionyesha nafsi yangu juu ya Ibn Abdi Kulal, hakuniitika katika lile ambalo nililitaka kwake nikaondoka na hali ya kuwa nina majonzi makubwa ninajiendea tu, sikuzinduka mpaka nilipofikn Qarni al-Thaalib, na hapa ndipo mahali ambapo siku Hizi panaitwa Qarni nl-Mzmazil. Nikakinyanyua kichwa changu na ghafla nikaona kiwingu kimetanda juu yangu, nikatazama na ndani yake nikamwona Jibril (Alayhi Salam), akaniita na kuniarnbia, ‘Kwa hakika Mwenyezi Mungu (ﷻ) Ameasikia maneno ya jamaa zako na yale ambayo wamekujibu na kwa Hakika Mwenyezi Mungu (ﷻ) Amekuletea Malaika wa majabali ili umuamrishe akufanyie jumbo lolote unalolitaka”, akaniita na Malaika wa majabali akanisalimia kisha akaniambia; “Ewe Muhammad mambo hayo ndivyo yalivyo unataka nini? Ukitaka niyakutanishe majabali mawili juu yao, wewe sema tu, maana nitafanya hivyo, (Al- akhshabaini hayo ni majabali mawili ya Makka Abu Qubasi na lile ambalo linaloelekeana nalo ni Quayqiaan) Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) akasema:
بل أرجو أن يُخْرِجَ اللَّهُ مِن أصلابِهِم مَن يعبدُ اللَّهَ ، لا يشرِكُ بِهِ شيئًا
“Mimi ninatarajia kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu kuwa kutoka migongoni mwao watatoka watu ambao watamwambudu Mwenyezi Mungu Peke Yake hali ya kuwa Hawamshirikishi na kitu chochote. ” (2)
Majibu aliyoyatoa Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷻ) ndiyo yanayodhihirisha kabisa Utume wake na yale ambayo alikuwa nayo miongoni mwa tabia njema na huruma ambayo haikufikiwa kina chake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alizinduka na moyo wake ukazizima kutokana na ushindi huu ambao ulikuwa ni jambo lililojificha kwake —- Ushindi huu aloteremshiwa na Allah (ﷻ) toka mbinguni. Mtume (ﷺ) aliendelea na safari yake kwa kurudi katika njia ya Makka mpaka alipofika katika jangwa la Nakhlah, hapa pana sehemu mbili ambazo zinafaa kwa kufanya makazi, As-Sayl Al-Kabir, na Az-Zziman, kwa kuwa sehemu hizi mbili zina maji na rutuba ya kutosha kwé kustawisha mimea.
Katika kufanya kwake makazi mahali hapa Mwenyezi Mungu (ﷻ) Alimpelékea kundi la majini ambao amewataja katika sehemu mbili ndani ya Qur’an katika Suratul Ahqaafi
وَإِذۡ صَرَفۡنَآ إِلَيۡكَ نَفَرٗا مِّنَ ٱلۡجِنِّ يَسۡتَمِعُونَ ٱلۡقُرۡءَانَ فَلَمَّا حَضَرُوهُ قَالُوٓاْ أَنصِتُواْۖ فَلَمَّا قُضِيَ وَلَّوۡاْ إِلَىٰ قَوۡمِهِم مُّنذِرِينَ (29) قَالُواْ يَٰقَوۡمَنَآ إِنَّا سَمِعۡنَا كِتَٰبًا أُنزِلَ مِنۢ بَعۡدِ مُوسَىٰ مُصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيۡهِ يَهۡدِيٓ إِلَى ٱلۡحَقِّ وَإِلَىٰ طَرِيقٖ مُّسۡتَقِيمٖ (30) يَٰقَوۡمَنَآ أَجِيبُواْ دَاعِيَ ٱللَّهِ وَءَامِنُواْ بِهِۦ يَغۡفِرۡ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمۡ وَيُجِرۡكُم مِّنۡ عَذَابٍ أَلِيمٖ (31)
[ Na wakati tulipo waleta kundi la majini kuja kwako kusikiliza Qur’ani. Basi walipo ihudhuria walisema: Sikilizeni! Na ilipo kwisha somwa, walirudi kwa kaumu yao kwenda kuwaonya. Wakasema: Enyi kaumu yetu! Sisi tumesikia Kitabu kilicho teremshwa baada ya Musa, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake, na kinacho ongoza kwenye Haki na kwenye Njia Iliyo Nyooka.Enyi kaumu yetu! Muitikieni Mwenye kuitia kwa Mwenyezi Mungu, na muaminini, Mwenyezi Mungu atakusameheni, na atakukingeni na adhabu chungu.] (46:29, 31)
Na kafika Surat Al-Jinni:
قُلۡ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ ٱسۡتَمَعَ نَفَرٞ مِّنَ ٱلۡجِنِّ فَقَالُوٓاْ إِنَّا سَمِعۡنَا قُرۡءَانًا عَجَبٗا (1) يَهۡدِيٓ إِلَى ٱلرُّشۡدِ فَـَٔامَنَّا بِهِۦۖ وَلَن نُّشۡرِكَ بِرَبِّنَآ أَحَدٗا (2)
[Sema: Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza, na likasema: Hakika sisi tumeisikia Qur’ani ya ajabu! Inaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu Mlezi.] mpaka ukamilifuwa aya ya kumina tano.
Kutokana na mtiririko wa aya hizi na kutokana na mtiririko wa mapokezi ambayo yamekuja katika kulitolea tafsiri tukio hili, kuwa Mtume (ﷺ) hakujua kuhudhuria kwa hilo kundi la majini na alilijua hilo baada ya Mwenyezi Mungu (ﷻ) kumfahamisha kupitia aya hizi. Ni wazi kuwa huko kuhudhuria kwao kulikuwa ni kwa mara ya kwanza. Mtiririko wa mapokezi unafahamisha kuwa baada ya hapa wao walikuja mara nyingi.
Ni kweli kuwa tukio hili lilikuwa ni ushindi mwingine ambao aliutoa Mwenyezi Mungu (ﷻ) kutoka katika khabari za ghaibu, mambo yaliyofichwa na askari wake ambao hakuna awajuaye isipokuwa Yeye. Kwa hakika katika aya zilizoshuka kuhusiana na tukio hili ndani yake kulikuwa na (bishara ya mafanikio ya Da’wa ya Mtume (ﷺ) na kuweka wazi kuwa hakuna nguvu yoyote katika nguvu za kilimwengu inayoweza kuzuia kufanikiwa kwa wito wake:
وَمَن لَّا يُجِبۡ دَاعِيَ ٱللَّهِ فَلَيۡسَ بِمُعۡجِزٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَيۡسَ لَهُۥ مِن دُونِهِۦٓ أَوۡلِيَآءُۚ أُوْلَٰٓئِكَ فِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٍ (32)
[Na wasio mwitikia Mwitaji wa Mwenyezi Mungu basi hao hawatashinda katika ardhi, wala hawatakuwa na walinzi mbele yake. Hao wamo katika upotovu ulio dhaahiri.] (46: 32)
وَأَنَّا ظَنَنَّآ أَن لَّن نُّعۡجِزَ ٱللَّهَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَن نُّعۡجِزَهُۥ هَرَبٗا (12)
[Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani, wala hatuwezi kumponyoka kwa kukimbia.] (72: 12)
Baada ya ushindi huu na bishara hizi, kiliondolewa kiwingu cha kukata tamaa, simanzi na huzuni iliyoufimika moyo wake tangu kurudi kwake kutoka Taif alikokuwa amefukuzwa na kurejea Makka. Alisimama na kuanza upya harakati zake za mwanzo katika kuutangaza Uislamu, na kuufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷻ) wa milele kwa uchangamfu, jitihada na hamasa mpya.
Wakati huo Zaidi bin Haritha (Radhi za Allah ziwe juu yake) alimwambia, ”Kwa vipi Utawafuata tena na hali ya kuwa wamekufukuza?’ Yaani hao Makuraishi. Mtume (ﷺ) akasema; “Ewe Zaid! kwa hakika kwa haya ambayo unayaona Mwenyezi Mungu Atatuletea faraja na matokeo mema, kwa hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) Atainusuru Dini Yake, na Atampa Ushindi Mtume Wake. “ Mjmnbe wa Mwenyezi Mungu (ﷻ) alikwenda mpaka alipokaribia kufika Makka akapiga kambi kafika mlima wa Hiraa na kisha akamtuma mtu mmoja kutoka katika ukoo wa Khuzaa aende kwa Al-Akhnas bin Shuraia akamuombe awe mdhamini wake. Akasema, ‘Mimi nimewekeana ahadi na watu wa Makka na mwenye kuweka ahadi hawezi kumdhamini mtu’, na yeye akapeleka ujumbe kwa Suhayli bin ’Amri akamueleza Suhayli; ’Kwa hakika watu wa ukoo wa ’Amir, hawatoi dhamana kwa watu wa ukoo wa Ka’ab.” Akapeleka ujumbe kwa Mut’im bin ’Adiyy, Mut’im akakubali. Alivaa silaha zake na kisha akawaita watoto wake, na jamaa zake akawaambia; ”Vaeni silaha zenu na mkakaé tayari mbele ‘ ya nguzo za Al-Ka’aba, kwani mimi nimemdhamini Muhammad“, na baada ya hapo akapeleka ujumbe kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) na kumuarifu kuwa anaweza kuingia Makka. Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) akaingia akiwa pamoja na Zaid bin Haritha (Radhi za Allah ziwe juu yake), alifululiza moja kwa moja mpaka alipofika ‘katika msikiti Mtukufu, Mut’im bin Adiyy akasimama juu ya mnyama wake, akatoa tangazo, ”Enyi jamaa miongoni mwa Makuraishi, kwa hakika mimi nimemdhamini Muhammad na kwa hivyo ninaomba mtu yeyote miongoni mwenu asimtie msukosuko.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) akasimama na kusali ‘rakaa mbili na baada ya hapo akaondoka na kuelekea nyumbani kwake, huku Al-Mutim bin Adiyy na watoto wake wamemzunguka wakiwa na silaha zao mpaka alipoingia nyumbani mwake.
Pamesemwa; Kwa hakika Abu Jahli alimwuliza Mut’im, ”Hivi wewe umechukua dhamana tu au ni mfuasi (Muislamu)?.” Akajibiwa; ”Hapana, nimemchukulia dhamana tu.” Akasema, ”Tumeikubalidhamana yako kwa yulé ambaye umemdhamini.” (3)
Kwa hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alikithamini sana kitendo hicho cha Mut’im, na ipo siku alisema kuhusiana na mateka wa Badri kuwa, _
لَوْ كَانَ المطعم بن عدي حياً، ثم كلمني في هؤلاء النتنى لَتركتهم له
[Laiti kamu Mut’im bin Adiyy angekuwa hai na kisha akanisemesha kuhusu hawa mateka wa Badri, basi ningeliwapa uhuru wao na kumkabidhi. (4)