ATAKAE KUFA NA ASIMJUE IMAMU WA ZAMA ZAKE BASI ATAKUFA KIFO CHA JAHILIA
Katika shubuhati za mashia katika kuithibitisha itikadi hii ya uimamu ni hadithi hii ambao utaipata katika vitabu vyote vya kishia
[من مات ولم يعرف إمام زمانه مات ميتة جاهلية]
[Atakae kufa na asimjue imamu wa zama zake atakufa kifo cha Jahilia.]
Na kudai kuwa hadihti hii iko katika vitabu vya ahlu Sunna.
Jawabu
Hadithi kwa tamko hilo au kwa swigha hii wanavyodai Mashia Hakuna katika vitabu vya Ahlu Sunnah.
Asema Sheikh Al-Albany Mungu amrehemu katika kitabu chake [Al-Silsilatul Ahadithi Dhwaifa wal-Maudhua 1/525].
“Atakae kufa na asimjue imamu wa zama zake atakufa kifo cha jahilia.”
Haina asili kwa lafdhi hii.
Na amesema Sheikhul-Isalaam Ibnu Taymia “Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu hajasema Mtume hivi,linalo julikana ni Hadithi ilio pokelewa na Imam Muslim kutoka kwa Ibnu Umar amesema nimemsika Mtume ﷺ akisema:
ما روى مسلم أن ابن عمر قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ” من خلع يدا من طاعة لقي الله يوم القيامة ولا حجة له، ومن مات وليس في عنقه بيعة مات ميتة جاهلية
[Atakae vua mkono wa utiifu (kwa kiongozi) atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa hana hoja,na atake kufa na hana katika shingo yake Bay’a atakufa kifo cha jahiliya.]
Kwa hivyo hadithi wanao dai Mashia haikupokewa kinamna hiyo wanavyo dai,bali wamebadilisha temko la Hadithi.
Kisha hata kama hadithi yao ni swahihi haina dalili juu ya itiadi yao ya kudai maimamu kumi na mbili.
Na kudai kwao kuwa hadithi hii iko katika vitabu vya Ahlu sunna ni kutaka kuwadanganya wenye ilimu chache kwa sabubu ya kufana matamshi yake.
Na hadithi inahimiza waislamu wawe watiifu kwa viongozi wao, na wasiwe niwenye kuasi.