باب الصلاة عَلَى الميت وتشييعه وحضور دفنه وكراهة اتباع النساء الجنائز
عن أَبي هُريرةَ رضيَ اللَّهُ وعنه أَنَّ رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قَالَ: “مَنِ اتَّبعَ جَنَازَةَ مُسْلمٍ إيمَاناً واحْتِسَاباً، وَكَانَ مَعَهُ حَتَّى يُصَلَّي عَلَيها ويَفْرُغَ مِنْ دَفنِها، فَإِنَّهُ يَرْجعُ مِنَ الأَجرِ بقِيراطَين كُلُّ قيرَاط مِثلُ أُحُدٍ، ومَنْ صَلَّى عَلَيهَا، ثُمَّ رَجَعَ قَبْلَ أَن تُدْفَنَ، فَإِنَّهُ يرجعُ بقِيرَاط” رواه البخاري
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
155. MLANGO WA KUMSWALIA MAITI, KUSINDIKIZA JENEZA LAKE, KUHUDHURIA MAZISHI YAKE NA UKARAHA WA WANAWAKE KUFWATA JENEZA
Imepokewa na Abû Huraira (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Mtume ﷺ amesema: “Atakayeliandama jeneza la Muislamu kwa kuamini na kutaraji ujira, akawa naye mpaka aswaliwe na amalize kuzikwa, hakika atarejea ana ujira wa Qirati mbili, kila Qirati ni mfano wa (jabali la) Uhud. Na atakayeliswalia kisha akarejea kabla hajazikwa, atarejea ana Qirati moja.” [ Imepokewa na Bukhari ]