[باب مَا يقوله مَن أيس من حياته]
عن عائشة، رضي اللَّه وعنها قالت: رأَيْتُ رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم وهُوَ بِالموتِ، عِندهُ قدحٌ فِيهِ مَاءٌ، وهُو يدخِلُ يدهُ في القَدَحِ، ثُمَّ يمسَحُ وجهَهُ بالماءِ، ثُمَّ يَقُولُ: “اللَّهُمَّ أَعِنِّي على غمرَاتِ الموْتِ وَسَكَراتِ المَوْتِ” رواه الترمذي.
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
147. MLANGO: DUA ANAYOOMBA ALIEKATA TAMAA YA KUISHI
Imepokewwa na ‘Âisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Nilimuona Mtume ﷺ naye yuko katika hali ya mauti, akiwa ana kikombe chenye maji, huku anaingiza mkono wake katika kikombe, kisha akiupangusa uso wake kwa maji na akisema: “Ewe Mola, Nisaidie katika shida za mauti na maumivu yake makali.” [ Imepokewa na Tirmidhy.]