[باب مَا يُدعى به للمريض]
عن عائشة، رضي اللَّه عنها أَن النبيَّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم كَانَ يعُودُ بَعْضَ أَهْلِهِ يَمْسَحُ بيدِهِ اليُمْنى ويقولُ: “اللَّهُمَّ ربَّ النَّاسِ، أَذْهِب الْبَأسَ، واشْفِ، أَنْتَ الشَّافي لاَ شِفَاءَ إِلاَّ شِفَاؤُكَ، شِفاءً لاَ يُغَادِرُ سقَماً” متفقٌ عَلَيْهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
145. MLANGO WA DUA ANAYOOMBEWA MGONJWA
Imepokewwa na ‘Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia kuwa, Mtume ﷺ alikuwa akimtembelea mmoja katika watu wake, akimpangusa kwa mkono wake wa kulia na akimwombea dua: “Allâhumma rabbannâs, adh-hibil-ba’s, washfi antasshâfî lâ shifâ-a illâ shifâ-uk, shifâ-allâyughâdiru saqamâ, [Ewe Mola Mlezi wa watu, Ondoa shida na maradhi, Ponya, Wewe Ndiwe Mponyaji, hakuna ponyo ispokuwa ni Lako, ponyo lisiloacha maradhi].” [ Wameafikiana Bukhârî na Muslimu ].