باب الرؤيا وَمَا يتعلق بها
وعن أبي هريرةَ رضي الله عنه أنَّ النبيَّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قَالَ: “إذَا اقتَربَ الزَّمَانُ لَمْ تَكَدْ رُؤْيَا الُمؤْمن تَكذبُ، وَرُؤْيَا المُؤْمِنِ جُزْءٌ منْ ستَّةٍ وَأرْبَعيَنَ جُزْءًا مِنَ النُبُوةِ ” متفقٌ عَلَيْهِ. وفي رواية: “أصْدَقُكُم رُؤْيَا: أصْدُقكُم حَديثاً“.
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
130. MLANGO WA NDOTO NA YANAYOFUNGAMANA NAYO
Imepokewa na Abû Huraira (Radhi za Allah ziwe juu yake) amepokea kutoka kwa Mtume ﷺ amesema: “Itakapokaribia mwisho wa zama, ndoto ya Mwumini haitakaribia kusema uwongo. Ndoto ya Mwumini ni sehemu katika sehemu arubaini na sita za Utume.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim ].
Riwaya nyingine imesema: “Mwenye ndoto ya kweli miongoni mwenu ni yule mwenye mazungumzo ya kweli.”