0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

781. Riyadhu Swalihina Mlango Wa  Sunna Ya Kuvaa Nguo Nyeupe Na Kujuzu Kuvaa Nguo Nyekundu Kijani Manjano Na Nyeusi Na Inajuzu Nguo Ya Pamba,Kitani….

باب استحباب الثوب الأبيض، وجواز الأحمر والأخضر والأصفر والأسود، وجوازه من قطن وكتان وشعر وصوف وغيرها إِلاَّ الحرير


وعن أَبي جُحَيفَةَ وَهْب بن عبد الله – رضي الله عنه -، قَالَ: رَأيتُ النبيَّ – صلى الله عليه وسلم – بِمكّةَ وَهُوَ بالأبْطَحِ في قُبَّةٍ لَهُ حَمْرَاءَ مِنْ أَدمِ، فَخَرَجَ بِلاَلٌ بِوَضُوئِهِ، فَمِنْ نَاضِحٍ وَنَائِلٍ، فَخَرَجَ النبيُّ – صلى الله عليه وسلم – وعليه حُلَّةٌ حَمْرَاءُ، كَأنِّي أنْظُرُ إِلَى بَيَاضِ سَاقَيْهِ، فَتَوَضّأ وَأذَّنَ بِلاَلٌ، فَجَعَلْتُ أتَتَبَّعُ فَاهُ هاهُنَا وَهَاهُنَا، يقولُ يَمِيناً وَشِمَالاً: حَيَّ عَلَى الصَّلاَةِ، حَيَّ عَلَى الفَلاَحِ، ثُمَّ رُكِزَتْ لَهُ عَنَزَةٌ، فَتَقَدَّمَ فَصَلَّى يَمُرُّ بَيْنَ يَدَيْهِ الْكَلْبُ وَالْحِمَارُ لاَ يُمْنَعُ.     متفقٌ عَلَيْهِ

{ العنَزة} بفتح النون: نحو العُكازَة


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Abû Juhaifah, Wahbi bin ‘Abdullâh (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Nilimuona Mtume ﷺ  Makkah naye yuko katika jangwa katika hema lake jekundu la ngozi. Bilâl akatoka na chombo chake chenye maji ya kutawadha, basi kulikuwa kuna wenye kunyunyiza na wenye kuchukua. Mtume ﷺ  akatoka naye amevaa nguo nyekundu. Kana kwamba (hivi sasa) natazama weupe wa miundi yake. Akatawadha, na Bilâl akaadhini. Nikawa naufatiliza kwa makini mdomo wake huku na huku; akisema – kuliani na kushotoni –: “Hayyâ ‘alassalâh, Hayyâ ‘alalfalâh.” Kisha akakitishiwa fimbo (iliokuwa na kichwa kidogo cha chuma), akatangulia na akaswalisha, mbele yake (fimbo) alikuwa akipita mbwa na punda wala hawafukuzwi.”   [ Wameafikiana Bukhari na Muslim ]


Begin typing your search above and press return to search.