باب العفو والإعراض عن الجاهلين
قَالَ الله تَعَالَى: ﴿خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بِالعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ الْجَاهِلينَ﴾ [ الأعراف: 199 ]
وقال تَعَالَى: ﴿فَاصْفَحِ الصَّفْحَ الْجَمِيلَ﴾ [ الحجر: 85 ]
وقال تَعَالَى: ﴿وَلْيَعْفُوا وَلْيَصْفَحُوا ألاَ تُحِبُّونَ أنْ يَغْفِرَ اللهُ لَكُمْ﴾ [ النور: 22 ]
وقال تَعَالَى: ﴿وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ وَاللهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنينَ﴾ [ آل عمران: 134 ]
وقال تَعَالَى: ﴿وَلَمَنْ صَبَرَ وَغَفَرَ إنَّ ذَلِكَ لَمِنْ عَزْمِ الأُمُورِ﴾ [ الشورى: 43 ]
والآيات في الباب كثيرة معلومة
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
75. MLANGO WA KUSAMEHE NA KUWAEPUKA MAJAHILI.
Mwenyezi Mungu Amesema: “Shikamana na kusamehe, na amrisha mema, na jitenge na majahili.” [7:199].
Mwenyezi Mungu Amesema:“Basi msamehe msamaha mzuri (kila anayekufanyia ubaya; malipo yenu mtayakuta huko Akhira).” [15:85].
Mwenyezi Mungu Amesema: “Na wasamehe, na waachilie mbali. Je! Nyinyi hampendi Allâh Awasamehe?” [24:22].
Mwenyezi Mungu Amesema: “Na wasamehevu kwa watu, na Allâh Huwapenda wafanyao mema.” [3:134].
Mwenyezi Mungu Amesema: “Na anayesubiri, na akasamehe, hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa.” [42:43].
Na Aya zinazoeleza mambo haya ni nyingi, mashuhuri.