باب إكرام الضيف
وعن أَبي شُرَيْح خُوَيْلِدِ بن عَمرو الخُزَاعِيِّ – رضي الله عنه -، قَالَ: سَمِعْتُ رسول الله – صلى الله عليه وسلم -، يقول: {مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَاليَوْمِ الآخِرِ فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ جَائِزَتَهُ} قالوا: وَمَا جَائِزَتُهُ؟ يَا رسول الله، قَالَ: {يَوْمُهُ وَلَيْلَتُهُ، وَالضِّيَافَةُ ثَلاَثَةُ أيَّامٍ، فَمَا كَانَ وَرَاءَ ذَلِكَ فَهُوَ صَدَقَةٌ عَلَيْهِ} متفقٌ عَلَيْهِ
وفي رواية لِمسلمٍ: {لاَ يَحِلُّ لِمُسْلِمٍ أنْ يُقِيمَ عِنْدَ أخِيهِ حَتَّى يُؤْثِمَهُ} قالوا: يَا رسول الله، وَكيْفَ يُؤْثِمُهُ؟ قَالَ: {يُقِيمُ عِنْدَهُ وَلاَ شَيْءَ لَهُ يُقْرِيه بِهِ}
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa na Abû Shuraih, Khuwailid bin ‘Amri al-Khuza‘iy (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Nilimsikia Mtume (ﷺ) akisema: “Anayemwamini Allâh na Siku ya mwisho amkirimu mgeni wake tunu yake.” Maswahaba wakauliza: “Yâ Rasûlallâh, tunu yake ni ipi?” Akawajibu: “Mchana wake na usiku wake. Ugeni ni siku tatu, inapozidi hapo, itakuwa ni sadaka.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim ] .
Riwaya nyingine ya Muslim imesema: “Si halali kwa Muislamu kuketi kwa nduguye (Muislamu) mpaka amtie katika dhambi.” Maswahaba wakauliza: “Yâ Rasûlallâh, atamtia vipi katika dhambi?” Akawajibu: “Aketi kwake naye (mwenyeji wake) hana kitu cha kumwandalia.”