0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

653. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Maamrisho kwa Watawala kuwafanyia upole Raia zao, kuwanasihi na Kuwahurumia..

باب أمر وُلاة الأمور بالرفق برعاياهم ونصيحتهم والشفقة عليهم والنهي عن غشهم والتشديد عليهم وإهمال مصالحهم والغفلة عنهم وعن حوائجهم


وعن أَبي يعلى مَعْقِل بن يَسارٍ – رضي الله عنه -، قَالَ: سَمِعْتُ رسول الله – صلى الله عليه وسلم -، يقول: { مَا مِنْ عَبْدٍ يَستَرْعِيهِ اللهُ رَعِيَّةً، يَمُوتُ يَوْمَ يَمُوتُ وَهُوَ غَاشٌّ لِرَعِيَّتِهِ، إِلاَّ حَرَّمَ اللهُ عَلَيْهِ الجَنَّة}   متفقٌ عليه

وفي رواية: { فَلَمْ يَحُطْهَا بِنُصْحِهِ لَمْ يَجِدْ رَائِحَةَ الجَنَّة}

وفي رواية لمسلم: { مَا مِنْ أميرٍ يلي أمور المُسْلِمينَ، ثُمَّ لا يَجْهَدُ لَهُمْ وَيَنْصَحُ لَهُمْ، إِلاَّ لَمْ يَدْخُلْ مَعَهُمُ الْجَنَّةَ}


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Abu Ya’lâ, Ma’qil bin Yasâr (Radhi za Allah ziwe juu yao) amesema: “Nilimsikia Mtume (ﷺ) akisema: “Mja yeyote aliejaaliwa na Allâh kuwaongoza raia, halafu siku ya kufa akafariki ilihali ni mwenye kuwaghushi raia wake, Allâh Atamharamishia Pepo!”       [ Wameafikiana Bukhari na Muslim].   

Riwaya nyingine imesema: “..wala hakuwahifadhi kwa kuwanasihi, basi hatanusa harufu ya Pepo!”

Riwaya nyingine ya Muslim imesema: “Amiri (kiongozi) yeyote anayesimamia mambo ya Waislamu, halafu asiwataabikie na kuwanasihi, hataingia Peponi pamoja nao.”


Begin typing your search above and press return to search.