KINGA YA MUISLAMU
[اللهم اسقنا غيثاً مغيثاً مريئاً مَريعاً نافعاً غير ضار ، عاجلاً غير آجل]
أبو داود 1/303 وصححه الألباني
[Ewe Mwenyezi Mungu tunyesheleze mvua yenye kuokoa, nyingi yenye kustawisha, yenye manufaa isiyo dhuru, ya haraka isiyochelewa.] [Imepokewa na Abuu Daud na kusahihishwa na Al-Baaniy]
[اللهم أغثنا ، اللهم أغثنا ، اللهم أغثنا]
البخاري 1/224 ،مسلم 2/613
[Ewe Mwenyezi Mungu tuokowe kwa kututeremshia mvua, ewe Mwenyezi Mungu tuokowe kwa kututeremshia mvua, ewe Mwenyezi Mungu tuokowe kwa kututeremshia mvua.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
[اللهم اسق عبادك وبهائمك ، وانشر رحمتك وأحيي بلدك الميت]
أبو داود 1/305 وحسنه الألباني
[Ewe Mwenyezi Mungu wanyesheleze waja wako, na wanyama wako, na eneza rehema zako nafufua nchi yako iliyokufa.] [Imepokewa na Abuu Daud na kuhasinishwa na Al-Baaniy.]
SIKILIZA DUA YA KUOMBA MVUA