باب حسن الخلق
وعن أَبي أُمَامَة الباهِليِّ – رضي الله عنه -، قَالَ: قَالَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم -: { أنَا زَعِيمٌ ببَيتٍ في ربَض الجَنَّةِ لِمَنْ تَرَكَ المِرَاءَ، وَإنْ كَانَ مُحِقّاً، وَبِبَيْتٍ في وَسَطِ الجَنَّةِ لِمَنْ تَرَكَ الكَذِبَ، وَإنْ كَانَ مَازِحاً، وَبِبَيْتٍ في أعلَى الجَنَّةِ لِمَنْ حَسُنَ خُلُقُهُ}. حديث صحيح، رواه أَبُو داود بإسناد صحيح
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Abû Umâmah al-Bâhily (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Mtume (ﷺ) amesema: “Mimi ni mdhamini wa nyumba kando ya Pepo kwa anayewacha mjadala hata kama ni mwenye haki, na ni mdhamini wa nyumba ilio katikati ya Pepo kwa anayewacha uwongo japo ni kwa mzaha, na ni mdhamini wa nyumba ilio mahala pa juu zaidi Peponi kwa ambaye tabia yake ni njema.” [ Imepokewa na Abû Dâwûd ameipokea kwa isnadi Sahîh.]