0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

56. MLANGO WA FADHILA YA NJAA, MAISHA YA CHINI, KUTOSHEKA KWA KICHACHE KATIKA VYAKULA, VINYWAJI, MAVAZI NA MENGINEYO KATIKA MAMBO YANAYOSTAREHESHA NAFSI, NA KUACHA MATAMANIO

 باب فضل الجوع وخشونة العيش والاقتصار عَلَى القليل من المأكول والمشروب والملبوس وغيرها من حظوظ النفس وترك الشهوات


قَالَ الله تَعَالَى: ﴿فَخَلَفَ منْ بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيّاً إِلاَّ مَنْ تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحاً فَأُولَئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ وَلاَ يُظْلَمُونَ شَيْئاً﴾ [ مريم: 59-60 ]

وقال تَعَالَى: ﴿فَخَرَجَ عَلَى قَوْمِهِ في زِينَتِهِ قَالَ الَّذِينَ يُريدُونَ الحَيَاةَ الدُّنْيَا يَا لَيْتَ لَنَا مِثْلَ مَا أُوتِيَ قَارُونُ إنَّهُ لَذُو حَظٍّ عَظِيمٍ وَقَالَ الَّذِينَ أُوتُوا العِلْمَ وَيْلَكُمْ ثَواب اللهِ خَيْرٌ لِمَنْ آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحَاً﴾ [ القصص: 79-80 ]

وقال تَعَالَى: ﴿ثُمَّ لًتُسْأَلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ النَّعِيمِ﴾ [ التكاثر: 8 ]

وقال تَعَالَى: ﴿مَنْ كَانَ يُريدُ العَاجِلَةَ عَجَّلْنَا لَهُ فِيهَا مَا نَشَاءُ لِمَنْ نُريدُ ثُمَّ جَعَلْنَا لَهُ جَهَنَّمَ يَصْلاَهَا مَذْمُوماً مَدْحُوراً﴾ [ الإسراء: 18 ]

والآيات في الباب كثيرةٌ معلومةٌ


شرح الحديث على آيات الباب مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



56. MLANGO WA FADHILA YA NJAA, MAISHA YA CHINI, KUTOSHEKA KWA KICHACHE KATIKA VYAKULA, VINYWAJI, MAVAZI NA MENGINEYO KATIKA MAMBO YANAYOSTAREHESHA NAFSI, NA KUACHA MATAMANIO


Mwenyezi Mungu Amesema: [ Lakini wakaja baada yao walio wabaya, wakaacha Swala, na wakafuata matamanio. Basi watakuja kuta malipo ya ubaya. Isipokuwa waliotubu, wakaamini, na wakatenda mema. Hao, basi, wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa chochote.]  [19:59, 60].

Mwenyezi Mungu Amesema:  [ Basi akawatokea watu wake katika pambo lake. Wakasema wale waliokuwa wanataka maisha ya kidunia: Laiti tungelikuwa tunayo kama aliyopewa Qaruni! Hakika yeye ni mwenye bahati kubwa. Na wakasema wale waliopewa ilimu: Ole wenu! Malipo ya Allâh ni bora kwa mwenye kuamini na akatenda mema.]  [28:79, 80].

Mwenyezi Mungu Amesema: [Kisha kwa hakika mtaulizwa siku hiyo juu ya neema (mlizopewa mlizitumiaje).]  [102:8].

Mwenyezi Mungu Amesema: [ Anayetaka yapitayo upesi upesi, Tutafanya haraka kumletea hapa hapa Tunayoyataka kwa Tumtakaye. Kisha Tumemwekea Jahannamu; ataingia humo hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa na kufurushwa.]  [17:18].


Begin typing your search above and press return to search.