0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

517. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Fadhila Ya Njaa, Maisha Ya Chini Kutosheka Kwa Vichache Katika Vyakula…..

 باب فضل الجوع وخشونة العيش والاقتصار عَلَى القليل من المأكول والمشروب والملبوس وغيرها من حظوظ النفس وترك الشهوات


وعن أَبي عبد الله جابر بن عبد الله – رضي الله عنهما -، قَالَ: بَعَثَنَا رسول الله – صلى الله عليه وسلم -، وَأمَّرَ عَلَيْنَا أَبَا عُبَيْدَةَ – رضي الله عنه -، نَتَلَقَّى عِيراً لِقُرَيْشٍ، وَزَوَّدَنَا جِرَاباً مِنْ تَمْرٍ لَمْ يَجِدْ لَنَا غَيْرَهُ، فَكَانَ أَبو عُبيدَةَ يُعْطِينَا تَمْرَةً تَمْرَةً، فَقيلَ: كَيْفَ كُنْتُمْ تَصْنَعُونَ بِهَا؟ قَالَ: نَمَصُّهَا كَمَا يَمَصُّ الصَّبي، ثُمَّ نَشْرَبُ عَلَيْهَا مِنَ الْمَاءِ، فَتَكْفِينَا يَوْمَنَا إِلَى اللَّيْلِ، وَكُنَّا نَضْرِبُ بِعِصيِّنَا الخَبَطَ، ثُمَّ نَبُلُّهُ بِالماءِ فَنَأكُلُهُ. قَالَ: وَانْطَلَقْنَا عَلَى سَاحِلِ الْبَحْرِ، فَرُفِعَ لَنَا عَلَى سَاحِلِ الْبَحْرِ كَهَيْئَةِ الكَثِيبِ الضَّخْمِ، فَأَتَيْنَاهُ فَإذَا هِيَ دَابَّةٌ تُدْعَى الْعَنْبَرَ، فَقَالَ أَبو عُبَيْدَةَ: مَيْتَةٌ، ثُمَّ قَالَ: لا، بَلْ نَحْنُ رُسُلُ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -، وفي سبيل الله وَقَدِ اضْطُرِرْتُمْ فَكُلُوا، فَأقَمْنَا عَلَيْهِ شَهْراً، وَنَحْنُ ثَلاَثُمِئَةٍ حَتَّى سَمِنَّا، وَلَقَدْ رَأيْتُنَا نَغْتَرِفُ مِن وَقْبِ عَيْنِهِ بِالقِلاَلِ الدُّهْنَ وَنَقْطَعُ مِنْهُ الفِدَرَ كالثَّوْرِ أَوْ كَقَدْرِ الثَّوْرِ، وَلَقَدْ أَخَذَ مِنَّا أَبو عُبَيْدَةَ ثَلاثَةَ عَشَرَ رَجُلاً فَأقْعَدَهُمْ في وَقْبِ عَيْنِهِ وَأخَذَ ضِلْعاً مِنْ أضْلاَعِهِ فَأقَامَهَا ثُمَّ رَحَلَ أعْظَمَ بَعِيرٍ مَعَنَا فَمَرَّ مِنْ تَحْتهَا وَتَزَوَّدْنَا مِنْ لَحْمِهِ وَشَائِقَ، فَلَمَّا قَدِمْنَا المَدِينَةَ أَتَيْنَا رسول الله – صلى الله عليه وسلم – فَذَكَرْنَا ذَلِكَ لَهُ، فَقَالَ: {هُوَ رِزْقٌ أخْرَجَهُ اللهُ لَكُمْ، فَهَلْ مَعَكُمْ مِنْ لَحْمِهِ شَيْءٌ فَتُطْعِمُونَا؟} فَأرْسَلْنَا إِلَى رسول الله – صلى الله عليه وسلم – مِنْهُ فَأكَلَهُ.     رواه مسلم


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Abû ‘Abdullâh, Jâbir bin ‘Abdullâh (Radhi za Allah ziwe juu yao) amesimulia: “Mtume   alitutuma (kwenda vitani), akatuekea Amiri awe ni Abû ‘Ubaidah (Radhi za Allah ziwe juu yake)  ili tukapambane na msafara wa Makureshi, akatupa akiba ya njiani mfuko wa tende, hakupata kingine cha kutupa ila hicho. Abû ‘Ubaidah akawa akitupatia tende moja-moja.” Akaulizwa: “Mlikuwa mkiifanyia nini tende hiyo (nayo ni moja)?” Akajibu: “Tulikuwa tukiinyonya kama vile mtoto anavyonyonya, kisha tukinywa maji, tende hiyo ikitutosha hadi usiku. Tulikuwa tukitikisa majani ya mti kwa fimbo zetu, kisha tukiyarowesha kwa maji na tukila. Tukatembea kando ya pwani ya bahari, tukaletewa hapo pwani ya bahari kitu kama mlima mkubwa. Tukakiendea, kumbe alikuwa ni mnyama anayeitwa nyangumi. Abû ‘Ubaidah akasema: “Huyu ni mfu.” Kisha akasema: “Hapana, bali sisi ni wajumbe wa Mtume  na tuko katika Njia ya Allâh, nanyi mmepatwa na shida kuu, kuleni.” Basi tukawa tunamla kwa mda wa mwezi mzima, nasi tulikuwa ni watu mia tatu, tulikula hata tukawanda. Twakumbuka, tulikuwa tukichota mafuta kutoka katika kishimo cha jicho lake na tukimkata minofu kama ukubwa wa ng’ombe. Abû ‘Ubaidah aliwachukua watu kumi na tatu kati yetu akawaketisha katika kishimo cha jicho lake, akachukua ubavu mmoja katika mbavu zake akausimamisha, akapitisha chini yake ngamia mrefu zaidi tuliekuwa naye na akapita chini yake. Tukachukua akiba ya minofu ya nyama yake. Tulipofika Madina, tulimwendea Mtume na tukamweleza habari hii. Akatwambia: “Hiyo ni riziki ambayo Allâh Amewatolea, je, mna kitu katika nyama yake mkatulisha nasi?” Tukampelekea Mtume nyama yake, akala.”    [ Imepokewa na Muslim.]

Begin typing your search above and press return to search.