0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

507. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Fadhila Ya Njaa, Maisha Ya Chini Kutosheka Kwa Vichache Katika Vyakula…..

 باب فضل الجوع وخشونة العيش والاقتصار عَلَى القليل من المأكول والمشروب والملبوس وغيرها من حظوظ النفس وترك الشهوات


وعن ابن عمر – رضي الله عنهما -، قَالَ: كُنَّا جُلُوساً مَعَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم -، إِذْ جَاءَ رَجُلٌ مِنَ الأنْصَارِ، فَسَلَّمَ عَلَيْهِ، ثُمَّ أدْبَرَ الأَنْصَاريُّ، فَقَالَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم -: {يَا أخَا الأنْصَارِ، كَيْفَ أخِي سَعْدُ بْنُ عُبَادَةَ؟} فَقَالَ: صَالِحٌ، فَقَالَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم -: {مَنْ يَعُودُهُ مِنْكُمْ؟} فَقَامَ وَقُمْنَا مَعَهُ، وَنَحْنُ بضْعَةَ عَشَرَ، مَا عَلَيْنَا نِعَالٌ، وَلاَ خِفَافٌ، وَلاَ قَلاَنِسُ، وَلاَ قُمُصٌ، نَمْشِي في تِلك السِّبَاخِ، حَتَّى جِئْنَاهُ، فَاسْتَأْخَرَ قَوْمُهُ مِنْ حَوْله حَتَّى دَنَا رسول الله – صلى الله عليه وسلم – وَأصْحَابُهُ الَّذِينَ مَعَهُ.     رواه مسلم


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa ‘Abdullâh bin ‘Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Tulikuwa tumeketi pamoja na Mtume ﷺ , mara akaja mtu katika Ansari, akamsalimia, kisha akaenda zake. Mtume ﷺ akamwuliza: “Ee ndugu wa Ansari, anaendeleaje ndugu yangu Sa’d bin Ubâdah?” Akamjibu: “Anaendelea vema.” Mtume ﷺ akatuuliza: “Ni nani atakayemtembelea kati yenu?” Akasimama, nasi tukasimama pamoja naye. Tulikuwa watu kumi na kitu hatuna viatu wala khuffu (aina ya kiatu cha ngozi chenye umbo la soksi) wala kofia wala kanzu, tukitembea katika ardhi kame. Tukamwendea (Sa’d), jamaa zake waliokuwa kando yake wakarudi nyuma, Mtume ﷺ na Maswahaba zake waliokuwa pamoja naye wakamkaribia      [ Imepokewa na Muslim ]

Begin typing your search above and press return to search.