باب فضل الزهد في الدنيا والحث عَلَى التقلل منها وفضل الفقر
وعن عبد الله بن مسعود – رضي الله عنه -، قَالَ: نَامَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – عَلَى حَصيرٍ، فَقَامَ وَقَدْ أثَّرَ في جَنْبِهِ، قُلْنَا: يَا رَسُولَ اللهِ، لَوْ اتَّخَذْنَا لَكَ وِطَاءً. فَقَالَ: {مَا لِي وَلِلدُّنْيَا؟ مَا أَنَا في الدُّنْيَا إِلاَّ كَرَاكِبٍ اسْتَظَلَّ تَحْتَ شَجَرَةٍ ثُمَّ رَاحَ وَتَرَكَهَا} رواه الترمذي، وقال: {حديث حسن صحيح}
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa ‘Abdullâh bin Mas‘ûd (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Mtume ﷺ alilala katika jamvi (mkeka), akaamka na lilikuwa limefanya athari ubavuni mwake. Tukamwambia: Yâ Rasûlallâh, waonaje lau tungalikutengenezea tandiko laini! Akasema: Sina haja ya dunia! Mimi katika dunia ni mfano wa msafiri aliejifunika chini ya kivuli cha mti kisha akaenda zake na akauwacha mti huo. [ Imepokewa na Tirmidhy, na amesema: Hadîth hii ni Hasan Sahîh.