باب فضل الزهد في الدنيا والحث عَلَى التقلل منها وفضل الفقر
وعن جابر – رضي الله عنه -: أنَّ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – مَرَّ بالسُّوقِ وَالنَّاسُ كَنَفَتَيْهِ، فَمَرَّ بِجَدْيٍ أَسَكَّ مَيِّتٍ، فَتَنَاوَلَهُ فَأَخَذَ بِأُذُنِهِ، ثُمَّ قَالَ: {أَيُّكُم يُحِبُّ أنْ يَكُونَ هَذَا لَهُ بِدرْهَم؟} فقالوا: مَا نُحِبُّ أنَّهُ لَنَا بِشَيْءٍ وَمَا نَصْنَعُ بِهِ؟ ثُمَّ قَالَ: {أَتُحِبُّونَ أَنَّهُ لَكُمْ؟} قَالُوا: وَاللهِ لَوْ كَانَ حَيّاً كَانَ عَيْباً، إنَّهُ أسَكُّ فَكَيْفَ وَهُوَ ميِّتٌ ! فقال: {فوَاللهِ للدُّنْيَا أهْوَنُ عَلَى اللهِ مِنْ هَذَا عَلَيْكُمْ} رواه مسلم
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka Jâbir (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Mtume ﷺ alipita sokoni na watu wameketi pambizoni mwake, akapita kwa mzoga wa mwana-mbuzi mwenye masikio mafupi, akalishika sikio lake na akauliza: [Ni nani anayependezwa kumnunua huyu kwa dirhamu?] Wakajibu: “Hatumtaki kwa thamani yoyote, kwani tutamfanyia nini? Akawaambia: Mwapendelea awe ni wenu? Wakajibu: Wallahi lau angalikuwa hai, ingalikuwa ni aibu kwa sababu ana masikio mafupi, basi itakuwaje naye ni mzoga? Akawaambia: Wallahi! Dunia ni duni mno kwa Allâh kuliko alivyo huyu mbele yenu. [ Imepokewa na Muslim.]