0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

456. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Fadhila Ya Kuipa mgongo Dunia, mahimizo ya kuwa nao kwa uchache na Fadhila ya ufukara.)

باب فضل الزهد في الدنيا والحث عَلَى التقلل منها وفضل الفقر


عن عمرو بن عوف الأنصاري – رضي الله عنه -: أنَّ رسولَ الله – صلى الله عليه وسلم – بَعَثَ أَبَا عبيدة بنَ الجَرَّاح – رضي الله عنه – إِلَى الْبَحْرَيْنِ يَأتِي بِجِزْيَتِهَا، فَقَدِمَ بمَالٍ مِنَ الْبَحْرَيْنِ، فَسَمِعَتِ الأَنْصَارُ بقُدُومِ أَبي عُبيْدَةَ، فَوَافَوْا صَلاَةَ الفَجْرِ مَعَ رسولِ الله – صلى الله عليه وسلم -، فَلَمَّا صَلَّى رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم -، انْصَرفَ، فَتَعَرَّضُوا لَهُ، فَتَبَسَّمَ رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم – حِيْنَ رَآهُمْ، ثُمَّ قَالَ: {أظُنُّكُمْ سَمعتُمْ أنَّ أَبَا عُبَيْدَةَ قَدِمَ بِشَيْءٍ مِنَ الْبَحْرَيْنِ؟} فقالوا: أجل، يَا رسول الله، فقال: {أبْشِرُوا وَأَمِّلْوا مَا يَسُرُّكُمْ، فَوالله مَا الفَقْرَ أخْشَى عَلَيْكُمْ، وَلكِنِّي أخْشَى أنْ تُبْسَط الدُّنْيَا عَلَيْكُمْ كَمَا بُسِطَتْ عَلَى مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ، فَتَنَافَسُوهَا كَمَا تَنَافَسُوهَا، فَتُهْلِكَكُمْ كَمَا أهْلَكَتْهُمْ}    متفقٌ عَلَيْهِ


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka Amru bin Awf al-Ansâry (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Mtume  ﷺ alimtuma Abû ‘Ubaidah bin al-Jarrâh (Radhi za Allah ziwe juu yake) Bahrain ili akachukue jizya (malipo makhsusi yanayolipwa na makafiri katika utawala wa Kiislamu ili kulipia usalama na haki wapewazo) ya huko. Akaja kutoka Bahrain na mali nyingi. Ansari wakasikia kuwa Abû ‘Ubaidah amekuja, wakahudhuria katika Swala ya asubuhi pamoja na Mtume ﷺ. Mtume ﷺ alipomaliza kuswali, aliondoka. Ansari wakamwendea wakimfahamisha haja zao. Mtume ﷺ alipowaona alitabasamu, kisha akawauliza: “Nadhani mmesikia kuwa Abû ‘Ubaidah amekuja na kitu kutoka Bahrain?” Wakajibu: “Ndio Yâ Rasûlallâh. (Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu)” Akawaambia: “Pokeeni bishara na mutarajie yatakayowafurahisha. Wallahi! Siwaogopei ufukara, lakini nawaogopea msije mkafunguliwa dunia kama walivyofunguliwa waliokuwa kabla yenu, mkaanza kuishindania kama walivyoishindania, na ikawa ndio sababu ya kuwaangamiza kama ilivyowaangamiza (wao).] .  [Wameafikiana Bukhari na Muslim.]


Begin typing your search above and press return to search.